Ubunifu wa kidijitali watajwa kuwa ni ufunguo wa mustakbali wa kibiashara barani Afrika

(CRI Online) Desemba 03, 2024

Wajumbe katika mkutano wa Jukwaa la Maendeleo ya Biashara Mwaka 2024 wametoa wito wa kuimarishwa kwa juhudi za kuhimiza ubunifu wa kidigitali kama njia ya kufungua mustakabali wa kibiashara barani Afrika.

Mkutano huo unafanyika mjini Kigali, Rwanda na kuandaliwa na TradeMark Africa (TMA), shirika la uungaji mkono wa kuhimza biashara barani Afrika kwa lengo la kuongeza ustawi wa Afrika kupitia biashara, kwa ushirikiano na serikali ya Rwanda.

Ukiwa unafanyika kwa lengo la kuangazia nguvu ya mageuzi ya ubunifu wa kidijitali, mkutano huo unafanyika chini ya kauli mbiu ya "Kufungua Mustakbali wa Biashara wa Afrika Kupitia Ubunifu wa Kidigitali”.

Akiongea kwenye mkutano huo, waziri wa biashara na viwanda wa Rwanda Bw. Prudence Sebahizi, amesisitiza jukumu muhimu la teknolojia kukabiliana na vizuizi vya kibiashara, kuhimiza uhusiano na kuwezesha ukuaji jumuishi wa uchumi.

Amesema kaulimbiu ya mwaka huu inaakisi matarajio ya Afrika kuijenga Afrika iliyounganishwa kidijitali na iliyo jumuishi kiuchumi, na wakati ambapo Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) linaendelea kuimarika, na teknolojia ikiwa ni injini itakayoendesha mageuzi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha