

Lugha Nyingine
China na Ujerumani zafanya mazungumzo ya kimkakati juu ya mambo ya diplomasia na usalama
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock wakiongoza kwa pamoja raundi ya saba ya Mazungumzo ya Kimkakati ya China na Ujerumani juu ya mambo ya Diplomasia na Usalama mjini Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 2, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock wameongoza kwa pamoja raundi ya saba ya Mazungumzo ya Kimkakati ya China na Ujerumani juu ya mambo ya Diplomasia na Usalama mjini Beijing siku ya Jumatatu ambapo, Wang amesema kuwa China imedumisha sera thabiti na tulivu kuhusu Ujerumani, na wakati wote imekuwa ikiichukulia Ujerumani kama mshirika wake muhimu wa ushirikiano tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 52 iliyopita.
Kuna tofauti kati ya China na Ujerumani, lakini tofauti hizo hazipaswi kuwa vikwazo kwa ushirikiano au sababu za mapambano, amesema Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).
Amesema China na Ujerumani zikiwa nchi zenye uchumi wa pili na wa tatu kwa ukubwa duniani, zinapaswa kushinda vikwazo, kutilia maanani mazungumzo na ushirikiano, kuachana na mawazo ya kizamani ya mapambano ya Vita Baridi, na kuepusha hatari za nje na kukabiliana na changamoto za kimataifa kwa pamoja.
Wang amesisitiza kuwa, ili kudumisha maendeleo tulivu ya uhusiano kati ya China na Ujerumani, ni lazima, kusawazisha kwanza maelewano ya kimkakati.
China ni nguvu ya amani, maendeleo na utulivu duniani, ikiwa na mwelekeo wa kimkakati na kisera wa wazi, wenye uwazi, Wang amesema, akiongeza kuwa, pande hizo mbili zinapaswa kutilia maanani kuheshimiana na kuelewana, na kufanya ushirikiano wa kunufaishana juu ya msingi huo.
Akibainisha maeneo mapana ya ushirikiano kati ya Ujerumani na China, Baerbock amesema Ujerumani inatilia maanani sana uhusiano wake na China na inafuata kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja.
Amesema, katika kukabiliana na dunia yenye misukosuko, kuna umuhimu mkubwa wa kudumisha mazungumzo ya wazi na kuimarisha mawasiliano ya kimkakati na China, ambayo inasaidia kudumisha mwelekeo sahihi wa maendeleo ya uhusiano wa pande mbili na kusaidia amani na utulivu wa dunia.
Amezungumza sana juu ya mchango wa China katika kushughulikia mabadiliko ya tabianchi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock wakiongoza kwa pamoja raundi ya saba ya Mazungumzo ya Kimkakati ya China na Ujerumani juu ya mambo ya Diplomasia na Usalama mjini Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 2, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma