Rais Xi Jinping akutana na Lee Hsien Loong na kutoa wito wa kuongeza ushirikiano kati ya China na Singapore

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 27, 2024

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mwandamizi wa Singapore Lee Hsien Loong kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, Novemba 26, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mwandamizi wa Singapore Lee Hsien Loong kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, Novemba 26, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Waziri Mwandamizi wa Singapore Lee Hsien Loong mjini Beijing siku ya Jumanne, akitoa wito wa kuoanisha zaidi mikakati ya maendeleo na kuongeza ushirikiano wa pande mbili.

Akipongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini Singapore katika wakati Bw. Lee alipokuwa waziri mkuu wa nchi hiyo, Rais Xi amesifu sana uungaji mkono wa muda mrefu wa Lee kwa ajili ya ushirikiano kati ya China na Singapore, amesema pande hizo mbili mwaka jana zilianzisha uhusiano wa wenzi wa pande zote, wa sifa bora na wa kuelekea mustakabali wa baadaye, zikiweka mwelekeo wa kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano wa pande mbili.

Rais Xi amesema kuwa mwaka ujao utakuwa wa maadhimisho ya miaka 35 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Singapore, ametoa wito kwa nchi hizo mbili kuimarisha mawasiliano kwenye ngazi ya juu, kuoanisha zaidi mikakati ya maendeleo, na kuzidisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani na ustawi wa kikanda.

Rais Xi amesema, China inaikaribisha Singapore kuendelea kuwa mtangulizi katika ushirikiano na China, kuhimiza miradi mikubwa ya ushirikiano, kutumia fursa zinazoletwa na maendeleo ya kidijitali na kijani, na kuandika ukurasa mpya kwenye ushirikiano wa pande mbili katika zama mpya.

Rais Xi amesema katika hali ya hatari na changamoto, hakuna hata nchi moja ni yenye kinga, ambapo kushikilia mshikamano, ushirikiano, uwazi na ujumuishaji ni njia sahihi ya kufuata nyayo.

Akikumbuka ziara yake ya China mwaka jana, Lee amesema uhusiano wa pande mbili tangu wakati huo umeimarishwa zaidi, na mkutano wa mfumo wa ushirikiano wa pande mbili umefanyika kwa mafanikio.

Amesema Singapore inajaa imani juu ya mustakabali wa China, akiongeza kuwa nchi hiyo itaendelea kuzidisha ushirikiano na China na kufanya juhudi za kushiriki katika ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.

Pande hizo mbili pia zimebadilishana maoni juu ya masuala makubwa yanayofuatiliwa kwa pamoja, kama vile uhusiano kati ya China na Marekani na hali ya kikanda.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mwandamizi wa Singapore Lee Hsien Loong kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, Novemba 26, 2024. (Xinhua/Li Xiang)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mwandamizi wa Singapore Lee Hsien Loong kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, Novemba 26, 2024. (Xinhua/Li Xiang)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha