Rais Xi akutana na Waziri Mkuu wa Samoa na kuahidi China kutoa kipaumbele kwa kuziwezesha nchi za Visiwa vya Pasifiki kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 27, 2024

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Samoa Fiame Naomi Mata'afa, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, Novemba 26, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Samoa Fiame Naomi Mata'afa, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, Novemba 26, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Waziri Mkuu wa Samoa Fiame Naomi Mata'afa mjini Beijing siku ya Jumanne, akisema China inapenda kuzisaidia nchi za Visiwa vya Pasifiki kupata uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi, kazi hii itapewa kipaumbele katika ushirikiano kati ya China na nchi hizo.

Rais Xi amemwambia Mata'afa kuwa, China itashirikiana na nchi za Visiwa vya Pasifiki katika kuhimiza utekelezaji kamili na wenye ufanisi wa “Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi” na “Makubaliano ya Paris”, kufuata kwa makini kanuni za wajibu wa pamoja lakini wenye tofauti ya kubebwa, kulinda haki na usawa, na maslahi ya pamoja ya Nchi za Kusini, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Rais Xi akidhihirisha kuwa Samoa ilikuwa moja kati ya nchi za kwanza za Visiwa vya Pasifiki kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya Watu wa China karibu miongo mitano iliyopita, na nchi mbili China na Samoa zimedumisha urafiki wa jadi, kuheshimiana, kutendeana kwa usawa na kufanya ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote.

Amesema China inaiunga mkono Samoa katika kulinda mamlaka ya nchi na uhuru wake, na kutafuta njia ya maendeleo inayofaa kwa hali halisi ya nchi yake.

“China itaendelea kutoa msaada kwa Samoa katika maendeleo yake ya uchumi na jamii , na kutumia kikamilifu nguvu na fursa katika uchumi, biashara, uwekezaji, kilimo na uvuvi ili kupata maendeleo kwa pamoja,” Rais Xi amesema.

Kwa upande wake Mata'afa amesema Samoa inatarajia kujifunza kutoka kwa uzoefu wa China katika kufikia ujenzi wa mambo ya kisasa, hasa katika kupunguza umaskini na kupata maendeleo ya kijani.

Huku akiishukuru China kwa msaada wake muhimu wa muda mrefu kwa Samoa, Mata'afa amesema Samoa inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na inaunga mkono Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia yaliyotolewa na Rais Xi.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Samoa Fiame Naomi Mata'afa, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, Novemba 26, 2024. (Xinhua/Li Xiang)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Samoa Fiame Naomi Mata'afa, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, Novemba 26, 2024. (Xinhua/Li Xiang)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha