Kitabu cha Xi Jinping kuhusu kujenga jeshi kwa mujibu wa sheria chachapishwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 25, 2024

BEIJING – Kitabu cha mkusanyiko wa maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) Xi Jinping kuhusu kujenga jeshi kwa mujibu wa sheria kimechapishwa, taarifa rasmi iliyotolewa jana Jumapili imeeleza.

Maelezo hayo yamenakiliwa kutoka kwenye hotuba na maandishi ya Rais Xi katika muda wa kuanzia Novemba 2012 hadi Juni 2024.

Kamati Kuu ya kijeshi imewataka maofisa na askari wa jeshi wa ngazi zote kusoma kwa kina kitabu hicho, na hasa imewataka maofisa waandamizi waoneshe umuhimu wao wa mfano wa kuigwa katika kuheshimu sheria, kusoma sheria, kufuata sheria na kutumia sheria.

Kupitia kusoma kitabu hicho, maofisa na askari wa jeshi wanatakiwa kuongeza uwezo wao wa kufikiria na kutenda kwa mujibu wa sheria katika kazi zao, hivyo kuharakisha mabadiliko ya kimsingi katika kazi ya kujenga jeshi na kuimarisha umuhimu wa utawala wa kisheria ili kuongeza uwezo wa ulinzi wa taifa na mambo ya kijeshi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha