Xi awasili Brasilia kwa ziara ya kiserikali nchini Brazil

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 20, 2024

Asubuhi ya Tarehe 19, Novemba kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China amewasili Brasilia kwa ziara ya kiserikali nchini Brazil.

Baada ya kuwasili uwanja wa ndege alilakiwa na Rui Costa, mkurugenzi wa ofisi ya Ikulu ya rais pamoja na maofisa wengine waandamizi wa Brazil, ambapo wasanii wanawake wa Bendi ya Batala walipiga muziki wa ngoma ulio wa furaha na uchangamfu kwa kumkaribisha.

Kabla ya kuwasili Brasilia, rais Xi alikuwa Rio de Janeiro, Brazil, kuhudhuria Mkutano wa 19 wa Viongozi wa kundi la G20.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha