Xi aelezea hatua 8 za China kwa ajili ya maendeleo ya dunia kwenye Mkutano wa G20

(CRI Online) Novemba 19, 2024

Rais Xi Jinping wa China Jumatatu alipotoa hotuba kwenye Mkutano wa 19 wa G20 kuhusu Mapambano Dhidi ya Njaa na Umaskini huko Rio de Janeiro, alielezea hatua nane za China kwa ajili ya maendeleo ya dunia.

Hatua hizo ni pamoja na kufanya ushirikiano wa ujenzi wa kiwango cha juu wa “Ukanda Mmoja Njia Moja”. Kutekeleza Pemdekezo la Maendeleo ya Dunia. Kuunga mkono maendeleo ya bara la Afrika. Kuunga mkono ushirikiano wa kimataifa kuhusu kupunguza umaskini na usalama wa chakula. Vilevile China, pamoja na Brazil, Afrika Kusini na Umoja wa Afrika, zimetoa pendekezo la Ushirikiano wa Kimataifa katika Uwazi wa Sayansiili kuhimiza mafanikio mapya ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia kunufaisha zaidi Nchi za Kusini.

Kuunga mkono G20 katika kutekeleza ushirikiano wa kivitendo kwa manufaa ya Nchi za Kusini na kutumia matokeo hayo kama Mwongozo wa Kuongeza Uwekezaji kwenye Nishati Safi katika Nchi Zinazoendelea na Kanuni za Kigezo cha Juu kuhusu Uchumi wa Kibiolojia kuwa na matokeo mazuri. Kutekeleza Mpango Kazi wa G20 wa Kupambana na Ufisadi, na pia China itakamilisha mfumo wa kiwango cha juu wa ufunguaji mlango kwa nje, na kufungua mlango wake zaidi kwa nchi zilizo za nyuma ya kimaendeleo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha