Kwa nini Bandari ya Chancay ya Peru inaitwa “Njia Mpya ya Ardhini na Baharini ya Asia-Latini Amerika katika Zama Mpya”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 15, 2024

Rais wa China Xi Jinping akihudhuria hafla kubwa ya ukaribisho iliyoandaliwa na Rais wa Peru Dina Boluarte kwenye uwanja mbele ya Ikulu ya Lima, Peru, Mchana wa tarehe 14, Novemba kwa saa za Peru. (Picha/People’s Daily)

Rais wa China Xi Jinping akihudhuria hafla kubwa ya ukaribisho iliyoandaliwa na Rais wa Peru Dina Boluarte kwenye uwanja mbele ya Ikulu ya Lima, Peru, Mchana wa tarehe 14, Novemba kwa saa za Peru. (Xinhua/Xie Huanchi)

Usiku wa Novemba 14 kwa saa za Peru, Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Peru Dina Boluarte walihudhuria hafla ya uzinduzi wa Bandari ya Chancay ya Peru kwa kupitia video.

"Kutoka Chancay hadi Shanghai, tunachoshuhudia siyo tu kukita mizizi na kustawi kwa Mpango wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' nchini Peru, bali pia kuzaliwa kwa njia mpya ya Ardhini na Baharini inayounganisha Asia na Latini Amerika katika zama mpya," amesema Rais Xi Jinping.

Hapo awali, Peru haikuwa na bandari ya kuweza kupokea meli kubwa za mizigo. Meli hizo zilihitaji kutia nanga Mexico na Panama, na sehemu nyingine kwa ajili ya kupita, na mizigo iliyokuwa inahitaji kwenda Peru, ilipakiwa kwenye meli ndogo kabla ya kupelekwa mpaka Peru.

Baada ya kukamilika kwa Bandari hiyo ya Chancay, gati lake litawezesha meli kubwa zenye uwezo wa kubeba makontena 18,000 kutia nanga, na muda wa usafirishaji wa baharini kutoka Lima, Peru hadi Shanghai, China utapungua kwa takriban siku 10.

Baadhi ya wasomi wa Peru wamesema Bandari ya Chancay inatarajiwa kuvutia uwekezaji mpya wa moja kwa moja kutoka nchi za nje, jambo ambalo litaimarisha maendeleo ya uchumi wa kikanda.

(Picha/People's Daily)

(Picha/People's Daily)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha