Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Peru

(CRI Online) Novemba 15, 2024

Rais Xi Jinping wa China akihudhuria hafla kubwa ya ukaribisho iliyoandaliwa na rais wa Peru kwenye uwanja mbele ya Ikulu ya Lima, Peru tarehe

Rais Xi Jinping wa China akihudhuria hafla kubwa ya ukaribisho iliyoandaliwa na Rais Dina Boluarte wa Peru kwenye uwanja mbele ya Ikulu ya Lima, Peru kabla ya mazungumzo. (Xinhua/Xie Huanchi)

wakifanya mazungumzo

Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Peru Dina Boluarte mjini Lima jana Alhamisi, Novemba 14. (Xinhua/Yao Dawei)

Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Peru Dina Boluarte mjini Lima jana Alhamisi, Novemba 14.

Rais Xi amesema katika kipindi cha miaka 53 iliyopita tangu China na Peru zianzishe uhusiano wa kidiplomasia, hasa tangu ziara yake ya kwanza nchini humo mwaka 2016, kwa juhudi za pamoja za pande zote mbili, thamani ya biashara na uwekezaji wa pande mbili imekua kwa kasi, ikileta manufaa kwa watu wa nchi hizo mbili.

Rais Xi amesema, pande zote mbili zinapaswa kujumuisha uzoefu wao, kuhimiza kiwango na hadhi ya ushirikiano kati ya China na Peru, kuimarisha biashara na uwekezaji kama vichocheo vya uchumi, kuhimiza maendeleo ya nyanja za kijadi na zile zinazoibuka, kuzidi kuunganisha minyororo ya viwanda na usambazaji, na kuhimiza kuinua hadhi ya ushirikiano wa kivitendo kati ya China na Peru na kati ya China na Latini Amerika.

Rais Xi ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Peru katika kujenga njia mpya ya ardhini na baharini kati ya China na Latini Amerika, na kufungua njia ya ustawi wa pamoja kwa Peru na vilevile kwa nchi za Latini Amerika na Caribean.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha