Marais wa China na Peru wahudhuria hafla ya kuzinduliwa kwa bandari ya Chancay

(CRI Online) Novemba 15, 2024

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China na Rais Dina Boluarte wa Peru wamehudhuria kwa pamoja hafla ya uzinduzi wa Bandari ya Chancay kwa njia ya video jana Alhamisi mjini Lima, Peru.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais Xi amesema bandari hiyo ya Chancay italeta faida kubwa kwa Peru na kutoa nafasi nyingi za ajira. Amesema, vilevile itaimarisha hadhi muhimu ya Peru katika kuunganisha Asia na Latini Amerika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha