Majaribio ya kikliniki ya kutengeneza chanjo dhidi ya mpox kuanza Kenya

(CRI Online) Novemba 14, 2024

Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kenya (KEMRI) imesema imesaini makubaliano ya ushirikiano na kampuni ya dawa ya Tonix ya Marekani, yenye lengo la kusanifu na kutekeleza majaribio ya kikliniki ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa mpox.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo mjini Nairobi, awamu ya kwanza ya majaribio hayo ya chanjo dhidi ya mpox ya TNX-801 yatafanyika nchini Kenya, yakilenga kutathmini usalama, uhimilivu na uwezo wa chanjo hiyo katika kuongeza kinga ya mwili dhidi ya ugonjwa huo.

Mkurugenzi Mkuu wa KEMRI, Elijah Songok amesema majaribio hayo pangwa ya chanjo yanaakisi juhudi za Kenya kuendeleza utafiti wa kisayansi ambao si tu utainufaisha Kenya, bali pia utachangia juhudi za kimataifa za kuzuia na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza yanayoibuka.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha