China yatangaza sera za kodi ili kuunga mkono soko la nyumba

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 14, 2024

Picha hii ikionyesha watu wakitazama meza ya mchanga ya mfano wa mradi wa nyumba mjini Shanghai, mashariki mwa China, Mei 28, 2024. (Xinhua/Zheng Juntian)

Picha hii ikionyesha watu wakitazama meza ya mchanga ya mfano wa mradi wa nyumba mjini Shanghai, mashariki mwa China, Mei 28, 2024. (Xinhua/Zheng Juntian)

BEIJING - China Jumatano imetangaza sera za kodi ili kuunga mkono maendeleo tulivu na mazuri ya soko la nyumba, hatua ambayo wachambuzi wanaamini itadumisha matarajio thabiti kuhusu sekta hiyo nguzo ambayo inashikilia ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.

Wizara ya Fedha ya China imesema nchi hiyo itaongeza motisha katika suala la kodi ya hati ya nyumba ili kuunga mkono kikamilifu mahitaji muhimu ya makazi ya watu na haja ya kuboresha hali zao za makazi.

Sera hizo mpya, ambazo zitaanza rasmi tarehe 1 Desemba 2024, zimeanzishwa kwa pamoja na Wizara ya Fedha ya China, Mamlaka ya Kodi ya Serikali ya China na Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Mijini na Vijijini ya China.

Watu wanaonunua nyumba yao pekee ya makazi au nyumba ya pili, mradi tu eneo hilo halizidi ukubwa wa mita za mraba 140, watalipa kodi ya hati ya nyumba kwa kiwango cha asilimia 1 kote nchini humo. Kwa nyumba zenye eneo linalozidi ukubwa wa mita za mraba 140, kodi hiyo itatozwa kwa kiwango cha asilimia 1.5.

Sera hiyo iliyorekebishwa kuhusu kodi ya hati ya nyumba itanufaisha hasa wale wanaopanga kununua nyumba kubwa zaidi, amesema Zhang Dawei, mchambuzi mkuu wa wakala wa nyumba, Centaline Property.

Wanunuzi wa nyumba wanaopanga kununua nyumba za pili mjini Beijing, Shanghai, Guangzhou na Shenzhen watafaidika zaidi na kodi hiyo ya hati uliorekebishwa, kwani kiwango cha awali cha asilimia 3 kitatumika kwa miji yote hiyo minne, Zhang amesema.

Chini ya sera hiyo mpya, wanunuzi wanaopanga kununua nyumba ya pili yenye eneo la sakafu la ukubwa wa mita za mraba 140 au chini ya hapo watafurahia kodi hiyo iliyopunguzwa ya asilimia 1, huku kwa wale wanaokusudia kununua nyumba za pili zenye eneo la sakafu la ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 140, kodi iliyorekebishwa ya hati imepunguzwa hadi asilimia 2.

Kwa kuzingatia uwezekano wa kuchunguza zaidi sera za soko la nyumba, Zhang ameongeza kuwa anatarajia sera zenye matokeo zaidi zitaendelea kutolewa katika siku zijazo -- ambazo zitasaidia kuleta utulivu wa matarajio ya soko la nyumba.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha