Rais Xi ajibu barua za watu marafiki wa China nchini Brazil

(CRI Online) Novemba 13, 2024

Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni alijibu barua za watu marafiki wa China kutoka makundi mbalimbali nchini Brazil, akiwahimiza kuchangia kila wakati katika urafiki kati ya China na Brazil.

Katika majibu yake, Rais Xi amesema kuwa anafurahi kuona kwamba urafiki kati ya China na Brazil umekuwa ukipitishwa kutoka kizazi hadi kizazi, akiongeza kuwa katika miaka 50 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, China na Brazil zimesonga mbele bega kwa bega, zikichangia taabu na raha, na zimeanzisha urafiki unaovuka milima na bahari.

Amesema kuwa China inapenda kufanya kazi na Brazil kuongeza urafiki kati ya nchi hizo mbili katika zama mpya, na kuufanya uhusiano kati ya China na Brazil kuwa mfano mzuri wa mshikamano, uratibu, maendeleo ya pamoja na kunufaishana kati ya nchi kubwa zinazoendelea, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa lengo kuu la amani na maendeleo ya binadamu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha