

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping aondoka Beijing kwa kuhudhuria mkutano wa APEC na kufanya ziara ya kiserikali nchini Peru
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 13, 2024
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ameondoka Beijing leo Novemba 13 kwa kuhudhuria Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi APEC huko Lima, Peru na kufanya ziara ya kiserikali nchini Peru kutokana na mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Peru Dina Ercilia Boluarte Zegarra.
Watu wanaoambatana na Rais Xi katika ziara yake hiyo ni Cai Qi, Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya CPC, na Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma