

Lugha Nyingine
Xi kuhudhuria mikutano ya APEC na G20 na kufanya ziara Peru na Brazil
(CRI Online) Novemba 08, 2024
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying ametangaza kuwa rais Xi Jinping wa China atahudhuria mkutano usio rasmi wa 31 wa wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki APEC mjini Lima na kufanya ziara nchini Peru kuanzia Novemba 13 hadi 17 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Peru Dina Ercilia Boluarte Zegarra.
Rais Xi pia atahudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa G20 huko Rio de Janeiro na kufanya ziara nchini Brazil kuanzia Novemba 17 hadi 21 kwa mwaliko wa Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma