

Lugha Nyingine
Idadi ya wafanyabiashara kutoka nje kwenye Maonyesho ya Biashara ya 136 ya Guangzhou yafikia rekodi mpya ya juu
Wafanyabiashara wa nchini na wa kutoka nje wakitembelea kwenye Maonyesho ya 136 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China ya Guangzhou (Picha iliyopigwa Oktoba 15).(Liu Dawei/Xinhua)
Maonyesho ya 136 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China yaliyofungwa Novemba 4 huko Guangzhou yalifikia rekodi mpya ya juu ambayo idadi ya wafanyabiashara wa manunuzi kutoka nje ilifikia 253,000, na idadi hiyo imezidi 250,000 kwa mara ya kwanza.
Takwimu hizo zilizotolewa na Kituo cha Biashara ya Nje cha China tarehe 4 zilijumuisha takwimu zilizotolewa hadi tarehe 3 Novemba, na zimefikia ongezeko la 2.8% zikilinganishwa na zile za maonyesho yaliyopita.
Wafanyabiashara wa manunuzi 253,000 wanatoka nchi na maeneo 214. Wanunuzi kutoka nchi zilizoshiriki katika ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" walifikia zaidi ya 60%, kwa jumla ni watu 165,000, ambao wameongezeka kwa 3.7%; idadi ya wanunuzi kutoka nchi za Mashariki ya Kati iliongezeka kwa kasi zaidi, na kufikia 34,000, ambayo ni ongezeko la 32.6%; idadi ya wanunuzi kutoka nchi za Ulaya na Marekani ilirudia kwa dhahiri, na watu 54,000 wameshiriki kwenye maonyesho hayo, ambayo imeongezeka kwa 8.2%.
Katika Maonyesho hayo ya Guangzhou, idadi ya kampuni kuu za manunuzi za kimataifa ilizidi 300 kwa mara ya kwanza, na kufikia 308. Thamani ya makubaliano ya uuzaji nje imefikia dola za Marekani bilioni 24.95, ambayo imeongezeka kuliko ile ya kwenye maonyesho yaliyopita. Kati yake, nchi zilizo za ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" zilifikia zaidi ya nusu, na makubaliano ya biashara kwenye masoko ya jadi ya Ulaya na Marekani yameongezeka.
Naibu mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Hali ya Nchi katika Chuo Kikuu cha Qinghua Bw.Yang Zhusong amesema, katika muktadha wa kuongezeka polepole kwa uchumi wa dunia na kudorora kwa biashara ya kimataifa, mafanikio mazuri hayo katika Maonyesho ya Guangzhou yanaonyesha mvuto mkubwa wa bidhaa bora zilizotengenezwa nchini China na imani ya jumuiya ya kimataifa kwa matarajio ya uchumi na ufunguzi mlango wa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma