

Lugha Nyingine
Hali ya hewa yaelezwa kuwa shwari kwa urushaji chombo cha Shenzhou-19 cha kubeba wanaanga kwenda anga ya juu
Picha hii iliyopigwa Oktoba 22, 2024 ikionyesha muunganisho wa chombo cha kubeba wanaanga kwenda anga ya juu cha Shenzhou-19 na roketi ya kurushia ya Long March-2F vikihamishwa kwa pamoja hadi kwenye eneo la urushaji. (Picha na Wang Jiangbo/Xinhua)
JIUQUAN - Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan kilichoko Kaskazini Magharibi mwa China kimetangaza kuwa hali ya hewa katika siku ya urushaji wa chombo cha China cha kubeba wanaanga kwenda kwenye anga ya juu, Shenzhou-19, itakuwa shwari, huku mazingira yote ya hali ya hewa yakikidhi mahitaji ya safari hiyo.
China itarusha chombo hicho katika siku za karibuni, huku uunganishaji wa chombo hicho na roketi ya kurushia ya Long March-2F vikiwa tayari vimeshahamishiwa kwenye eneo la urushaji.
Chombo hicho kimekamilisha ukaguzi wake wa mwisho kabla ya kurushwa, na ukaguzi wa mfumo mzima wa kudhibiti upitishaji hewa. Roketi hiyo na chombo hicho cha Shenzhou-19 vimekamilisha majaribio ya ufanisi wa umeme, na wanaanga na mifumo yote kwenye eneo la urushaji, na kufanya mazoezi ya utayari wa urushaji, huku kila kitu kikiripotiwa kuwa katika hali nzuri.
Ren Fengjie, afisa wa idara ya hali ya hewa ya kituo hicho, amesema kazi hiyo ya urushaji itafanyika mwishoni mwa majira ya mpukutiko na mapema katika majira ya baridi, huku kukiwa na joto la chini wakati wa usiku kwenye eneo la urushaji.
Amesema, wafanyakazi wa hali ya hewa wameanza ukaguzi wa hali ya vifaa muhimu tangu mwezi mmoja uliopita, na kufanya mapitio ya kihistoria na uchambuzi maalum wa hali ya hewa juu ya upepo mkali, mvua na joto.
“Katika siku za hivi karibuni, wameendelea kufuatilia hali ya hewa na kuchambua data za hali ya hewa kwa wakati halisi. Kwa mujibu wa mabadiliko ya hali ya hewa kwenye eneo la urushaji na maeneo ya jirani, wameweka msingi imara wa utabiri wa hali ya hewa kwa "dirisha la urushaji" na kutoa huduma sahihi na za kuaminika za hali ya hewa ili kusaidia kazi ya urushaji,” amesema Ren.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma