China yaandaa mkutano wa kuhamasisha matumizi ya mfumo wake wa urambazaji wa BeiDou

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 25, 2024

Picha ya droni iliyopigwa Oktoba 24, 2024 ikionyesha eneo la maonyesho ya wazi la Mkutano wa 3 wa Kimataifa wa Matumizi ya BDS (Mfumo wa Satalaiti ya Urambazaji wa BeiDou) mjini Zhuzhou, Mkoa wa Hunan, Katikati mwa China. (Xinhua/Cheng Ji'an)

CHANGSHA - Mkutano wa 3 wa Kimataifa wa Matumizi ya BDS (Mfumo wa Satalaiti ya Urambazaji wa BeiDou) umeanza Alhamisi mjini Zhuzhou, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, wakati ambapo idara husika za serikali ya China zikilenga kuhamasisha tasnia hiyo kwa kupanua matumizi na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.

Mkutano huo wa siku mbili umevutia watafiti, wafanyabiashara na maafisa wa China na wa nchi za nje zaidi ya 1,800. Waonyeshaji pia wameweka mabanda ya kuonyesha matumizi ya programu za BDS katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na usambazaji unaotumia teknolojia za kisasa na usafirishaji wa kisasa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha