Rais Xi arejea Beijing baada ya kuhudhuria mkutano wa 16 wa viongozi wa nchi za BRICS

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 25, 2024

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amerejea Beijing Alhamisi usiku baada ya kuhudhuria Mkutano wa 16 wa Viongozi wa Nchi za BRICS uliofanyika Kazan, Russia kuanzia Oktoba 22 hadi 24.

Msafara wa Rais Xi, ambao ni pamoja Cai Qi, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati Kuu ya CPC, na Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China, umerejea kwa ndege moja.

Kabla ya Rais Xi kuondoka Kazan, maafisa wa Russia walimuaga kwenye uwanja wa ndege.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha