Rais Xi ahimiza nchi za "BRICS Plus" kutafuta usalama na maendeleo ya pamoja na mapatano kati ya ustaarabu mbalimbali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 25, 2024

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu yenye kichwa "Kuunganisha Nguvu Kubwa ya Nchi za Kusini Kujenga Pamoja Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja" kwenye mazungumzo ya viongozi wa nchi za "BRICS Plus"  huko Kazan, Russia, Oktoba 24, 2024. (Xinhua/Li Xueren

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu yenye kichwa "Kuunganisha Nguvu Kubwa ya Nchi za Kusini Kujenga Pamoja Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja" kwenye mazungumzo ya viongozi wa nchi za "BRICS Plus" huko Kazan, Russia, Oktoba 24, 2024. (Xinhua/Li Xueren)

KAZAN, Russia - Rais Xi Jinping wa China jana Alhamisi alipokuwa akihutubia katika mazungumzo ya viongozi wa "BRICS Plus" ametoa wito kwa nchi za "BRICS Plus" kujitahidi kwa ajili ya usalama wa pamoja, maendeleo ya pamoja na mapatano kati ya ustaarabu mbalimbali.

Akidhihirisha kuwa kujitokeza kwa pamoja kwa Nchi za Kusini ni umaalumu wazi wa mageuzi makubwa duniani kote, Rais Xi amesema, Nchi za Kusini kusonga mbele pamoja kuelekea ujenzi wa mambo ya kisasa ni tukio kubwa sana katika historia ya dunia na haijawahi kutokea katika ustaarabu wa binadamu.

Wakati huo huo, amani na maendeleo bado vinakabiliwa na changamoto kubwa, na njia ya kuuelekea ustawi kwa Nchi za Kusini haitakuwa nyoofu, amesisitiza, huku akihimiza nchi za "BRICS Plus" kutumia hekima na nguvu za pamoja, kuwa na ujasiri wa kubeba wajibu wao, na kuhimiza kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Rais Xi amesema kuwa nchi za "BRICS Plus" zinapaswa kulinda amani na kujitahidi kupata usalama wa pamoja, kujitokeza mbele kwa pamoja ili kuunda nguvu ya kuleta amani na utulivu, kuimarisha usimamizi wa usalama wa dunia, na kutafuta suluhu za kushughulikia vyote dalili na vyanzo vya kusababisha matatizo makubwa.

Pande nyingi zimeitikia kwa hamasa Pendekezo la Usalama wa Dunia alilopendekeza. "Chini ya Pendekezo hilo, tumepata maendeleo dhahiri katika kudumisha utulivu wa kikanda na katika maeneo mengine mengi," Rais Xi amesema, akiongeza kuwa China na Brazil zilitoa kwa pamoja maoni sita ya pamoja, na zikijiunga pamoja na nchi nyingine za kusini zimeanzisha kikundi cha Marafiki wa Amani kwa mgogoro wa Ukraine.

Amesema kuwa tangu kutolewa kwa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia miaka mitatu iliyopita, limesaidia kupatikana kwa dola za Kimarekani karibu bilioni 20 za mfuko wa maendeleo na kuzindua miradi zaidi ya 1,100. Na hivi karibuni Jumuiya ya Kimataifa AI ya Viwanda na Kituo cha Ubora wa Uundaji Bidhaa kimeanzishwa Shanghai.

Akisisitiza kwamba ustaarabu mbalimbali ni ubora wa asili wa dunia, Rais Xi ametoa wito kwa nchi za "BRICS Plus" kuhimiza kwa pamoja maendeleo ya ustaarabu wote na hali ya mapatano kati yao, kuwa watetezi wa mabadilishano kati ya ustaarabu mbalimbali, na kuimarisha mawasiliano na mazungumzo.

Rais Xi Jinping wa China akipiga picha pamoja na viongozi na  wajumbe wengine waliohudhuria mazungumzo ya viongozi wa nchi za "BRICS Plus"  huko Kazan, Russia, Oktoba 24, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)

Rais Xi Jinping wa China akipiga picha pamoja na viongozi na wajumbe wengine waliohudhuria mazungumzo ya viongozi wa nchi za "BRICS Plus" huko Kazan, Russia, Oktoba 24, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha