

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atetea maendeleo makubwa ya hali ya juu ya ushirikiano wa BRICS
Rais Xi Jinping wa China akihutubia Mkutano wa 16 wa Viongozi wa nchi za BRICS huko Kazan, Russia, Oktoba 23, 2024. Mkutano huo umeandaliwa na Rais wa Russia Vladimir Putin, na kuhudhuriwa na Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva (kwa njia ya video), Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan. (Xinhua/Xie Huanchi) (Xinhua/Xie Huanchi)
KAZAN, Russia - Rais Xi Jinping wa China jana Jumatano wakati akihutubia Mkutano wa 16 wa Viongozi wa nchi za BRICS uliofanyika Kazan, Russia ambao uliendeshwa na Rais wa Russia Vladimir Putin, ametoa wito kwa nchi za BRICS kufanya juhudi kwa ajili ya ushirikiano mkubwa zaidi wa nchi za BRICS na maendeleo ya hali ya juu ya jumuiya hiyo.
Kwenye mkutano wa kikundi kikundi, Rais Xi amekaribisha nchi wanachama wapya kwenye familia ya BRICS na kualika nchi nyingi kuwa nchi washirika.
Rais Xi amesema kuwa upanuzi wa jumuiya ya BRICS ni mnara mkubwa katika historia yake ya maendeleo, na ni tukio la alama katika mabadiliko ya hali ya kimataifa. Amesema nchi za BRICS zimekuja pamoja ni kwa ajili ya utafutaji wao wa pamoja na kwa kufuata mwelekeo mkuu wa amani na maendeleo.
Xi amesisitiza kwamba Dunia inapitia mabadiliko makubwa ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita, yakiwa na mwelekeo mpya wa dunia yenye ncha nyingi na hatari ya "Vita Baridi vipya," nchi za BRICS zinapaswa kutumia fursa ya kihistoria, kuchukua hatua za mapema, kushikilia nia ya awali na majukumu ya ufunguaji mlango, jumuishi, na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote, kufuata mwelekeo wa jumla wa kuibuka kwa Nchi za Kusini, kutafuta maoni ya pamoja huku zikiweka pembeni tofauti, kufanya juhudi kwa pamoja ili kuimarisha zaidi maadili ya pamoja, kulinda maslahi ya pamoja, na kuimarisha nchi za BRICS kwa kupitia mshikamano.
"Lazima tufanye juhudi kwa pamoja ili kuzijenga nchi za BRICS kuwa njia kuu ya kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya Nchi za Kusini na kuwa watangulizi katika usimamizi na mageuzi ya dunia nzima ," Rais Xi amesema.
Amezihimiza nchi za BRICS kufuata kwa pamoja njia ya maendeleo, kutetea utandawazi wa uchumi wa dunia wenye manufaa kwa wote na jumuishi, na kushikilia kanuni ya maendeleo kwa pamoja.
Amesema nchi za BRICS zinapaswa kuimarisha msingi wa ushirikiano, kuendeleza kwa kina ushirikiano katika sekta za jadi za kilimo, nishati, madini, uchumi na biashara, kupanua ushirikiano katika maeneo yanayoibukia kama vile maendeleo ya kijani, yenye kutoa kaboni chache na akili mnemba, na kulinda biashara, uwekezaji na usalama wa mambo ya fedha.
Rais huyo wa China kisha alihudhuria mkutano wa kundi kubwa, akatoa hotuba muhimu kuhusu maendeleo ya siku za baadaye ya BRICS na kutoa mapendekezo matano.
Xi amesema, "Wakati Dunia inaingia katika kipindi kipya chenye msukosuko na mabadiliko , tunakabiliwa na machaguo muhimu ambayo yatajenga maisha yetu ya baadaye. Je, turuhusu Dunia kujitumbukiza kwenye shimo la kina kirefu la machafuko na kutokuwa na utaratibu, au tujitahidi kuirejesha katika njia ya amani na maendeleo?" Rais Xi amesema.
Rais Xi ametoa wito kwa nchi za BRICS kushikilia kanuni tatu muhimu: kutopanua medani ya vita, kutopamba moto wa migogoro, na kutofanya uchocheaji wa moto kwenye migogoro, na kujitahidi kupunguza haraka hali ya mgogoro wa Ukraine.
Rais Xi Jinping wa China akihutubia Mkutano wa 16 wa Viongozi wa nchi za BRICS huko Kazan, Russia, Oktoba 23, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)
Viongozi wa BRICS wakipiga picha pamoja huko Kazan, Russia, Oktoba 23, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma