Rais Xi Jinping ampongeza Luong Cuong kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Vietnam

(CRI Online) Oktoba 23, 2024

Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa Luong Cuong kwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Vietnam.

Rais Xi amesema katika miaka ya hivi karibuni amedumisha mawasiliano ya karibu ya kimkakati na viongozi wa Vietnam, na kuongoza kwa pamoja uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuingia kwenye zama mpya ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa umuhimu wa kimkakati.

Amesema, China inaiunga mkono kithabiti Vietnam kufuata njia ya ujamaa inayoendana na hali halisi ya nchi na katika kujiandaa kwa mkutano mkuu wa 14 wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam.

Ameongeza kuwa, anatilia maanani sana kuendeleza uhusiano kati ya China na Vietnam, na yuko tayari kufanya kazi na Luong Cuong kuongoza na kuzidisha ujenzi wa jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja, na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha