Rais Xi Jinping aondoka Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 16 wa Viongozi wa BRICS nchini Russia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 22, 2024

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping leo Jummane ameondoka Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 16 wa Viongozi wa BRICS utakaofanyika Kazan, Russia kutokana na mwaliko wa Rais wa Shirikisho la Russia Vladimir Putin.

Watu wanaoambatana na Rais Xi katika safari hii ni Cai Qi, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya CPC, na Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha