

Lugha Nyingine
Biashara ya malighafi, vipuri na bidhaa kati ya China na Afrika yaongezeka kwa asilimia 6.4 mwezi Januari-Julai
BEIJING - Biashara kati ya China na Afrika katika malighafi, vipuri na bidhaa iliongezeka kwa asilimia 6.4 mwaka hadi mwaka katika miezi saba ya kwanza ya Mwaka 2024, takwimu rasmi zilizotolewa jana Jumanne zimeonyesha.
Ofisa wa Idara kuu ya Forodha ya China Bw. Lu Daliang amesema, Biashara ya malighafi, vipuri na bidhaa kati ya China na Afrika inachukua asilimia 68 ya thamani ya jumla ya biashara ya pande hizo mbili, ikiisaidia Afrika katika mchakato wake wa maendeleo ya viwanda na kuufanya uchumi kuwa wa aina mbalimbali.
Katika kipindi cha Januari hadi Julai, biashara ya pande mbili ilifikia thamani ya jumla ya yuan trilioni 1.19 (dola za Kimarekani karibu bilioni 166.48), huku mauzo ya China barani Afrika yakifikia yuan bilioni 697.93, wakati uagizaji wa China wa bidhaa kutoka Afrika ulifikia yuan bilioni 490.89, takwimu hizo za forodha zimebainisha.
Mkutano wa Kilele wa Mwaka 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utafanyika Beijing kuanzia Septemba 4 hadi 6, na kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili kunatarajiwa, Lyu amesema.
Kaulimbiu ya mkutano wa FOCAC wa Mwaka 2024 ni "Kushikana Mikono Kuhimiza Ujenzi wa Mambo ya Kisasa na Kujenga Jumuiya ya Ngazi ya Juu ya China na Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja," tangazo lililotolewa na wizara ya mambo ya nje ya China Julai 30 linasema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma