Kisima cha kwanza cha gesi katika kimo kidogo cha maji kwa ukubwa duniani, kwenye maji ya kina kirefu baharini kina gesi ya mita za ujazo zaidi ya bilioni 100

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 08, 2024

Picha hii isiyo na tarehe iliyotolewa na CNOOC ikionyesha kisima cha gesi cha Lingshui 36-1 katika maji ya bahari kusini mashariki mwa Hainan, mkoa wa kisiwa ulioko kusini zaidi mwa China. (CNOOC/ Xinhua)

Picha hii isiyo na tarehe iliyotolewa na CNOOC ikionyesha kisima cha gesi cha Lingshui 36-1 katika maji ya bahari kusini mashariki mwa Hainan, mkoa wa kisiwa ulioko kusini zaidi mwa China. (CNOOC/ Xinhua)

BEIJING – Kiasi cha Gesi asili iliyopo (OGIP) katika kisima cha gesi cha Lingshui 36-1 – ambacho ni kisima cha kwanza cha gesi katika kimo kidogo cha maji kwa ukubwa duniani, kwenye maji ya kina kirefu baharini - kimekadiriwa kuwa na mita za ujazo zaidi ya bilioni 100, Shirika la Taifa la Mafuta ya Baharini la China (CNOOC) limesema.

CNOOC, moja ya kampuni tatu kubwa za mafuta za China, siku ya Jumatano ilisema kwamba mamlaka husika ya serikali imeidhinisha data hiyo.

Kisima cha gesi cha Lingshui 36-1 kiko katika maji ya baharini kusini mashariki mwa Hainan, mkoa wa kisiwa ulioko kusini zaidi mwa China.

Kampuni hiyo imekadiria kuwa OGIP ya mabonde ya Yinggehai, Qiongdongnan na Zhujiangkou katika Bahari ya Kusini ya China ni mita za ujazo zaidi ya trilioni 1.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha