

Lugha Nyingine
China yaitaka Marekani kutatua masuala ya ndani ya haki za binadamu na kuacha kuingilia mambo ya nchi nyingine
BEIJING - China inaitaka Marekani kushughulikia ipasavyo matatizo yake mengi ya haki za binadamu, badala ya mara kwa mara kutumia haki za binadamu kama kisingizio cha kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine na kutumia fimbo kubwa ya vikwazo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian amesema siku Jumatano.
Lin ameyasema hayo kwenye mkutano na wanahabari akijibu vizuizi vya kiholela vya viza vya Marekani dhidi ya maafisa wa China.
Lin amesema kuwa Marekani inaeneza habari za uwongo kimakusudi, inadharirisha hali ya haki za binadamu ya China, inaweka vizuizi vya kiholela vya viza dhidi ya maafisa wa China, inaingilia sana mambo ya ndani ya China, na inakiuka sana sheria za kimataifa na kanuni za msingi zinazosimamia uhusiano wa kimataifa.
"China inapinga vikali hili, na imewasilisha malalamiko kwa upande wa Marekani," Lin amesema.
“Kama hatua ya kulipiza, China, kwa mujibu wa sheria, itaweka vizuizi vya visa kama hivyo kwa maafisa wa Marekani wanaotunga uongo juu ya masuala ya haki za binadamu kuhusiana na China, kuhimiza kuanzishwa kwa vikwazo dhidi ya China na kuharibu maslahi ya China,” ameongeza.
Akibainisha Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa (UN) limeidhinisha kwa kauli moja ushiriki wa China katika duru ya nne ya Mapitio ya Kila Baada ya Kipindi Maalum ya Nchi Wanachama Wote (UPR) si muda mrefu uliopita, Lin amesema hii inaonyesha wazi kwamba jumuiya ya kimataifa inakubali sana mafanikio ya China katika haki za binadamu.
"Marekani haina haki ya kutoa maoni juu ya hali ya haki za binadamu ya nchi nyingine na kutoa kauli za kutowajibika," Lin amesema, akiongeza kuwa jumuiya ya kimataifa kwa muda mrefu imekuwa ikiona wazi na kuchukizwa na unyanyasaji wa haki za binadamu unaofanywa na Marekani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma