Ziara ya Rais Xi katika Asia ya Kati ni muhimu kwa ushirikiano, maendeleo ya kikanda: Waziri wa Mambo ya Nje wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2024

BEIJING – Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema siku ya Jumamosi kwamba, ziara ya Rais Xi Jinping wa China ambayo imemalizika hivi karibuni katika Asia ya Kati ina umuhimu mkubwa kwa kuongoza mwelekeo wa maendeleo ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), kuzidisha uhusiano wa urafiki na ujirani mwema kati ya China na nchi za kikanda, na kuhimiza kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya nchi jirani.

Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu mahudhurio ya Rais Xi kwenye Mkutano wa 24 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa SCO mjini Astana, na ziara za kiserikali nchini Kazakhstan na Tajikistan wiki hii.

Rais Xi alihudhuria mkutano wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa SCO pamoja na mkutano wa SCO+, na kusema kwamba SCO inasimama upande sahihi wa historia, haki na usawa, na ina umuhimu mkubwa kwa Dunia, Wang amesema.

Rais wa China ametoa wito kwa SCO, ambayo inakabiliwa na hali mpya na changamoto mpya, kuhakikisha usalama, kulinda haki za maendeleo, kuimarisha nguvu ya mshikamano, na kujitahidi kujenga maskani ya pamoja ya kushikamana na kuaminiana, kuwa na amani na utulivu, ustawi na maendeleo, ujirani mwema na urafiki, pamoja na haki na usawa, Wang amesema.

Akijulisha ziara ya Rais Xi nchini Kazakhstan, Wang amesema wakuu wa nchi mbili za China na Kazakhstan wamesisitiza nia yao thabiti ya kisiasa ya kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya China na Kazakhstan yenye mustakabali wa pamoja, na kufanya mipango mipya ya kuingia "miaka 30 ya dhahabu" mipya ya uhusiano wa pande mbili.

Wakati alipojulisha ziara ya Rais Xi nchini Tajikistan, Wang ameeleza kuwa, tokea zama mpya, rais wa China amekutana na Rais wa Tajikistan Emomali Rahmon mara 15. Akisema kuwa katika ziara ya safari hii ya Rais Xi, viongozi wakuu wa nchi hizo mbili wametangaza kuanzishwa kwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote katika zama mpya kati ya China na Tajikistan, na kujenga pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwenye hatua ya mwanzo ya juu zaidi. Wang amesema, wakati wa kuhudhuria kwa Rais Xi kwenye mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa SCO mjini Astana, rais pia alifanya mkutano wa pande mbili mbili kati yake na Rais wa Russia Vladimir Putin na viongozi wa nchi nyingine waliohudhuria kwenye mkutano huo.

Viongozi hao wa nchi mbalimbali wameelezea matumaini yao ya kujifunza kutoka kwa uzoefu wa utawala wa China na kuharakisha mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa wa nchi zao, Wang amesema.

Wang amesema, viongozi hao wa nchi mbalimbali wamesema wazi kwamba wanashikilia kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na kupinga “Taiwan ijitenge” kwa aina yoyote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha