

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping akutana na Rais Aliyev wa Azerbaijan
Rais Xi Jinping wa China akikutana na rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan. (Picha na Yue Yuewei/Xinhua)
Mchana wa Tarehe 3, Julai kwa saa za Kazakhstan, rais Xi Jinping wa China alikutana na rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan kabla ya kuhudhuria kwenye Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Astana, Kazakhstan.
Xi alisema, China na Azerbaijan ni marafiki wazuri wa dhati na wanaoaminiana na ni wenzi wa kufanya ushirikiano wa kunufaishana kwa usawa. Uhusiano kati ya China na Azerbaijan siku zote unaendelea vizuri kwa utulivu, na ushirikiano wa nchi hizo mbili umepata matunda kemkem na kuhusisha mambo mengi zaidi ya kimkakati. Tumepandisha uhusiano wa pande hizo mbili kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati, ambao ni nafasi mpya na pia ni mwanzo mpya. Pande zetu mbili zinapaswa kuendelea kuungana mkono, ili kuwanufaisha vizuri zaidi watu wa nchi zetu mbili.
Xi Jinping alisisitiza kuwa, China inaunga mkono kithabiti juhudi za Azerbaijan za kulinda mamlaka ya nchi, uhuru na ukamilifu wa ardhi yake, na inaiunga mkono kutafuta njia ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya nchi yake. Pande zote mbili zinatakiwa kusukuma ushirikiano wa kujenga pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kwenye kiwango cha juu, kuendeleza kwa kina ushirikiano katika biashara, uwekezaji, mafuta na gesi, nishati ya jua n.k., kuimarisha mafungamano ya mawasiliano, kujenga vizuri njia ya usafirishaji ya kimataifa ya kuvuka Caspian, na kuhakikisha Treni kati ya China na Ulaya zinaendeshwa vizuri kwa utulivu.
Aliyev alisema, Azerbaijan na China ni washirika wazuri. Mawasiliano ya karibu yamedumishwa kati ya idara mbalimbali na kwenye ngazi mbalimbali za nchi hizo mbili, thamani ya biashara kati yao imekuwa ikiongezeka siku hadi siku, na zinaungana mkono kithabiti katika kulinda uhuru na mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi katika jumuiya za kimataifa. Leo, tumetoa taarifa ya pamoja inayotangaza kuanzisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya Azerbaijan na China, ambayo ina umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili. Azerbaijan inashikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja, na inashikilia kuunga mkono juhudi za China za kuhimiza muungano wa taifa, ambalo ni mkondo wa kihistoria usioweza kuzuiliwa na nguvu yoyote. Azerbaijan ingependa kuimarisha mshikamano na ushirikiano na China, kutafuta fursa, na kuimarisha ushirikiano katika biashara, uwekezaji, nishati mpya, na utamaduni ndani ya mfumo wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".
Pande hizo mbili zilitoa "Taarifa ya Pamoja ya Jamhuri ya Watu wa China na Jamhuri ya Azerbaijan kuhusu Kuanzisha Uhusiano wa Wenzi wa Kimkakati."
Idara husika za pande hizo mbili zilitia saini nyaraka za ushirikiano kuhusu kujenga pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na mafungamano ya mawasiliano kati ya nchi hizo mbili.
Rais Xi Jinping wa China akikutana na rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan. (Picha na Yue Yuewei/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma