Ushirikiano wa BRI unakumbatia mwelekeo wa kihistoria wa utandawazi wa kiuchumi: Wataalam

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 22, 2024

Wataalamu kutoka Bangladesh na China wakihudhuria mkutano wa majadiliano huko Dhaka, Bangladesh, Mei 20, 2024. (Xinhua)

Wataalamu kutoka Bangladesh na China wakihudhuria mkutano wa majadiliano huko Dhaka, Bangladesh, Mei 20, 2024. (Xinhua)

DHAKA - Ushirikiano wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) unaendana na mwelekeo wa kihistoria wa utandawazi wa kiuchumi, unaitikia wito wa kuboresha mfumo wa usimamizi wa kimataifa, na unakidhi matarajio ya watu kwa maisha bora ambayo ni sababu kuu ya kwa nini umekuwa na nguvu siku zote, wamesema wataalamu wa Bangladesh.

Makumi ya wazungumzaji kutoka sekta mbalimbali nchini Bangladesh na China, ikiwa ni pamoja na taaluma, biashara na vyombo vya habari, wameeleza maoni yao katika mkutano wa majadiliano uliofanyika Dhaka, Bangladesh siku ya Jumatatu, wakisema kwamba Bangladesh ni mshiriki wa kujivunia wa BRI ambayo inatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi hiyo.

Kituo cha mfuko wa Asia Mashariki (CEAF), ambacho ni taasisi huria ya taaluma isiyo na faida na isiyo ya kisiasa, umeandaa mkutano wa kujadili mada ya "Uhusiano kati ya China na Bangladesh na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja" katika Chuo Kikuu cha Dhaka.

Nasim Mahmmud, mkurugenzi mtendaji wa CEAF, akihutubia mkutano huo amesema China siku zote imeunga mkono kithabiti Bangladesh katika kulinda mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi, na kupinga uingiliaji wa nchi za nje.

Amesema uhusiano kati ya Bangladesh na China unajenjgwa juu ya kuheshimiana na kunufaishana.

Mkuu wa Kitivo cha Mafunzo ya Biashara katika Chuo Kikuu cha Dhaka Muhammad Abdul Moyeen amesema kwamba Bangladesh tayari imenufaika na BRI, ikiwa ni pamoja na uwekezaji wa kifedha wa China.

Pia amesema uwekezaji unaofanywa na BRI utaendelea kuchangia maendeleo ya uwezo wa kushindana wa Bangladesh katika siku zijazo na utekelezaji kikamilifu wa Dira ya 2041.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhusiano wa Kimataifa kutoka Akademia ya Sayansi ya Jamii ya Shanghai, Wang Jian amesema, BRI imehimiza maendeleo ya Bangladesh, kwa kuboresha miundombinu yake kama barabara, madaraja na uzalishaji wa umeme, pamoja na ukuaji wa biashara kati ya China na Bangladesh.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha