

Lugha Nyingine
Balozi wa China aionya Uingereza kutohatarisha uhusiano zaidi
LONDON - Balozi wa China nchini Uingereza Zheng Zeguang amekutana na ofisa husika wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza siku ya Jumanne, na kuionya Uingereza isiende mbali zaidi katika njia hatari ya kuhatarisha uhusiano kati ya China na Uingereza.
Kwenye mkutano huo, Zheng alitoa malalamiko kwa upande wa Uingereza juu ya tabia yake potofu, ikiwa ni pamoja na shutuma zake zisizo na msingi dhidi ya serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong, na kukanusha visingizio vilivyotolewa na upande wa Uingereza.
Balozi huyo ameweka wazi kwamba Uingereza lazima ikomeshe njama za kisiasa dhidi ya China na isiende mbali zaidi katika njia hatari ya kuhatarisha uhusiano kati ya China na Uingereza.
Uingereza siku ya Jumatatu ilibumba kile kinachoitwa kesi ili kuipaka matope na kushambulia serikali ya Hong Kong, Zheng amesema huku akiongeza kuwa, kwa muda sasa, Uingereza imeandaa mlolongo wa shutuma dhidi ya China, zikiwemo zile za "majasusi wa China" na mashambulizi ya mtandaoni.
"Tuhuma zote hizo hazina msingi na ni za kashfa. Upande wa Uingereza pia umekuwa ukinyanyasa, kukamata na kuweka kizuizini raia wa China nchini Uingereza kwa kisingizio cha kisheria na usalama wa taifa. Hii ni sawa na uchochezi mkubwa dhidi ya China na inakiuka vikali kanuni za msingi zinazosimamia uhusiano wa kimataifa. Haikubaliki kabisa," amesema.
Hong Kong imerejea nchi mama yake China kwa muda mrefu na Uingereza haina haki na haina nafasi ya kunyooshea vidole na kuingilia kati masuala ya Hong Kong, balozi huyo amesema.
Serikali ya China bado inaendelea kuwa na nia thabiti katika kupambana na wahusika wanaoipinga China wanaotaka kuivuruga Hong Kong na katika kudumisha utulivu na ustawi wa mkoa huo, amesema huku akiongeza kuwa, Uingereza kuhifadhi wahalifu wanaosakwa ni kukanyaga utawala wa sheria na hakutafanyikiwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma