

Lugha Nyingine
Rais Xi aipongeza Nauru kwa kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru
(CRI Online) Februari 01, 2024
Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa mwenzake wa Nauru David Adeang siku ya Jumatano kufuatia nchi hiyo kuadhimisha miaka 56 tangu ipate uhuru wake.
Kwenye salamu zake, Rais Xi amesema China na Nauru tayari zimerejesha uhusiano wa kibalozi, na zinafungua ukurasa mpya wa uhusiano wao. Amemsifu Rais Adeang kwa kufanya uamuzi wa kisiasa wenye busara wa kutambua sera ya kuwepo kwa China moja.
Rais Xi ameeleza kutilia maanani kuendeleza uhusiano kati ya China na Nauru na anapenda kufanya juhudi na Rais Adeang, kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, kuhimiza ushirikiano wa kivitendo na mabadilishano ya kitamaduni ili kunufaisha watu wa nchi hizo mbili.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma