

Lugha Nyingine
Uwekezaji wa China wawezesha ukuaji wa nishati mpya nchini Zimbabwe
Waziri wa Maveterani wa Mapambano ya Ukombozi wa Zimbabwe Bw. Christopher Mutsvangwa amesema, utaalamu wa China katika teknolojia ya nishati mpya na uwekezaji wa makampuni yake nchini Zimbabwe unaiwezesha nchi hiyo kuwa mshiriki muhimu katika mageuzi ya kijani duniani.
Waziri huyo amesema katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua yaliyochapishwa siku ya Jumanne kwamba, Zimbabwe inatumia uwezo wa kiviwanda wa China kuelekea katika kuhamia kwenye nishati mpya duniani, na kwamba inakaribisha uwekezaji kutoka China.
Bw. Mutsvangwa amesema kutokana na miradi mikubwa ya uchakataji wa madini ya lithium iliyowekezwa na China, Zimbabwe inapiga hatua ya kuonesha mchango mkubwa katika mnyororo wa thamani wa lithiamu duniani.
Mwezi Desemba mwaka jana, serikali ya Zimbabwe ilipiga marufuku uuzaji wa lithium ghafi nje ya nchi, ili kuhamasisha uwekezaji katika miundo mbinu ya viwanda vya uchakataji ya nchini humo. Pia iliidhinisha sera ya madini ya lithium ili kuimarisha mkakati wa madini wa nchi hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma