

Lugha Nyingine
Meli ya "Xuelong 2" yaenda kwenye bahari ya Amundsen kufanya utafiti wa kisayansi
Tarehe 5, Desemba, meli ya “Xuelong 2” ikivunja barafu ili kuweka njia kwa safari ya meli ya kubeba mizigo ya "Tianhui". (Zhou Yuan/Xinhua)
Mchana wa tarehe 25 kwa saa za Beijing, meli ya “Xuelong 2” inayofanya utafiti wa 40 wa China katika eneo la Ncha ya Kusini ya Dunia ilimaliza kazi ya kuongeza ugavi wa mahitaji na mabadilishano ya watafiti ikiondoka Bandari ya Lyttelton nchini New Zealand na kuelekea Bahari ya Amundsen ili kufanya utafiti wa kisayansi.
Katika kipindi kijacho, meli hiyo itakwenda kwenye Bahari ya Amundsen kufanya uchunguzi wa jumla kuhusu hali ya viumbe hai, mazingira ya hewa ya anga ya juu, mazingira ya bahari, na hali ya kutapakaa kwa vitu vya uchafuzi, ambapo pia itasaidia kazi ya miradi nyingine ya utafiti wa kisayansi ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma