

Lugha Nyingine
Kampuni ya Huawei ya China yawatunuku vyeti wanafunzi wa Tanzania
Kampuni ya Teknolojia na Mawasiliano ya China Huawei imefanya hafla ya kuwatunuku vyeti wanafunzi wa Tanzania walioshiriki kwenye programu yake iitwayo Seeds for the Future (SFTF) mjini Dar es Salaam jana Jumatatu.
Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari wa Tanzania Bw. Nape Nnauye, amepongeza uungaji mkono wa Huawei katika kuandaa vijana wenye vipaji katika nyanja ya habari, mawasiliano na teknolojia (TEHAMA), akisema hii ndiyo misukumo mikuu kwa mageuzi ya kidijitali na uchumi yanayotegemea utaalamu.
Bw. Nnauye amesema hayo wakati aliwapotunuku vyeti wanafunzi wa vyuo vikuu walioshiriki kwenye programu ya SFTF, iliyoanzishwa mwaka 2016 nchini Tanzania kwa lengo la kuhimiza maendeleo ya TEHAMA na kuchangia utimizwaji wa mpango wa uchumi wa kidijitali wa nchi hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma