

Lugha Nyingine
Tanzania yapata nafasi ya obiti na kufungua njia ya kurushwa kwa satelaiti ya kwanza katika anga ya juu
Tanzania imepata nafasi muhimu katika obiti na kufungua njia ya kurusha satelaiti yake ya kwanza katika anga ya juu.
Mafanikio hayo ya kihistoria yaliyotangazwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Tanzania, Nape Nnauye, yanaashiria hatua kubwa ya nchi hiyo katika kusonga mbele kuelekea malengo yake ya anga ya juu.
Habari hizi zinakuja baada ya Bw Nnauye kuwahakikishia Watanzania mwezi Julai juu ya dhamira isiyoyumba ya serikali ya Tanzania kurusha katika anga ya juu satelaiti kuu ya nchi hiyo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja ujao, akisema serikali inaamini hilo na kwa sasa inaweka msingi.
Uwezo wa kifursa wa satelaiti ya Tanzania ni mkubwa. Sekta kama vile mawasiliano, kilimo, usimamizi wa maafa, na viwanda husika zitanufaika sana kutokana na uwezo wake. Zaidi ya hayo, teknolojia hii itatumika kwenye utafutaji wa maliasili na sekta nyingine muhimu za kiuchumi.
Katika bara zima la Afrika, ni mataifa machache tu yanayotumia uwezo wa teknolojia ya satelaiti. Misri inaongoza kwa kuwa imesharusha katika obiti ya anga ya juu satelaiti tisa, ikifuatiwa na Afrika Kusini (nane), Algeria (saba), na Nigeria (sita). Nchi nyingine kama Morocco, Ghana, Kenya, Rwanda, na Mauritius zimejiunga na mataifa yanayorush vyombo kwenye anga ya juu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma