Huawei yazindua programu ya "Mbegu za Baadaye" nchini Botswana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 22, 2023

Wanafunzi wakihudhuria uzinduzi wa mpango wa Huawei wa Mwaka 2023 wa "Mbegu za Baadaye  " (Seeds for the Future) mjini Gaborone, Botswana, Novemba 21, 2023. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Wanafunzi wakihudhuria uzinduzi wa mpango wa Huawei wa Mwaka 2023 wa "Mbegu za Baadaye" (Seeds for the Future) mjini Gaborone, Botswana, Novemba 21, 2023. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

GABORONE - Kampuni ya kiteknolojia ya China, Huawei imezindua programu ya “Mbegu za Baadaye” (Seeds for the Future) siku ya Jumanne nchini Botswana, ikilenga kukuza vipaji vya wenyeji vya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) na viongozi vijana kwa ajili ya siku za baadaye na kuendeleza maendeleo ya jumuiya za kidijitali.

Wanafunzi takriban 25 wa shahada ya kwanza kutoka vyuo vikuu vinne nchini Botswana wameanza kushiriki mtandaoni katika programu hiyo kuanzia Novemba 21 hadi 27. Kwenye programu hiyo, wanafunzi watapata uzoefu mzuri, ikiwa ni pamoja na mihadhara ya kiufundi, warsha za uongozi, uzoefu wa utamaduni wa China na mawasiliano na wenzao kutoka sehemu mbalimbali duniani, amesema David Zhang, Mkurugenzi Mkuu wa Huawei nchini Botswana, ambaye alifungua rasmi hafla hiyo katika mji mkuu wa Botswana, Gaborone.

"Pia watashiriki katika shughuli ya kimataifa ya Huawei ya Uwajibikaji wa Kijamii, "Tech4Good", na kutafuta njia za namna teknolojia ya TEHAMA inavyoweza kusaidia kushughulikia masuala makubwa yanayowakabili binadamu," Zhang ameongeza.

Kila mwaka, Huawei huwaalika wanafunzi kujadili mwelekeo wa baadaye na kuwataka watumie vizuri fursa mpya kama sehemu ya mpango wake mkuu wa Uwajibikaji kwa Jamii.

Washindi wa shindano hili la kimataifa wataalikwa China kwa ajili ya Shindano la Uvumbuzi la Tech4Good, ambapo watatembelea Shenzhen, Beijing na miji mingine ya China ili kujifunza kuhusu mifumo ya kijasiriamali ya dunia na kushindania kupata dola za Kimarekani 100,000 kutoka mfuko wa usaidizi wa kuanzisha shughuli za kijasiriamali.

Waziri wa Vijana, Jinsia, Michezo na Utamaduni wa Botswana Tumiso Rakgare amesema TEHAMA ni kiwezeshaji muhimu cha maendeleo ya nchi hiyo katika kujenga jamii yenye maarifa, elimu, ukuaji wa uchumi, utawala na uvumbuzi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha