

Lugha Nyingine
Saa za mikono zenye Utarizi wa Hariri wa Suzhou zadumsiha ustadi wa jadi wa Mashariki ya Dunia
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 16, 2023
Sanaa ya utarizi wa hariri wa Mji wa Suzhou ni moja ya aina nne maarufu zaidi za utarizi wa hariri nchini China. Tangu sanaa hiyo ilipowekwa kumbukumbu kwa mara ya kwanza kwenye waraka wa historia wa kipindi cha Madola Matatu ya China (B.K. 220-280), imerithishwa kwa zaidi ya miaka elfu moja. Mwaka 2006, sanaa ya utarizi wa hariri wa Suzhou iliorodheshwa kuwa urithi wa kitaifa wa utamaduni usioshikika wa China.
Kampuni ya saa ya FIYTA ya Shenzhen, China imetia sanaa hiyo nzuri ya kijadi kwenye usanifu wa saa za mikono, na kuunganisha teknolojia ya kisasa ya saa na ustadi wa utarizi wa hariri wa Suzhou wenye mvuto, ikidumisha ustadi huo wa jadi wa Mashariki ya Dunia bila ya kujali kubadilika kwa wakati.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma