Misri kuzalisha megawati 1200 za umeme kupitia kinu cha nyuklia

(CRI Online) Novemba 15, 2023

Mamlaka ya udhibiti wa nyuklia ya Misri imetoa kibali cha kuanzisha kitengo cha nne na cha mwisho katika kinu cha nyuklia cha El-Dabaa, chenye uwezo wa kuzalisha megawati 1200 za umeme.

Katika taarifa yake, Mamlaka ya Udhibiti wa Nyuklia na Radiolojia ya Misri (ENRRA) ilisema iliidhinisha mchakato wa ujenzi huo baada ya ukaguzi wa kina kuanzia Oktoba 21 hadi Novemba mosi, kipindi kitakapokamilika, kituo hicho kinatarajiwa kusaidia Misri kuzalisha umeme zaidi kwa matumizi ya viwandani na pia kwenye maeneo ya kibiashara na makazi.

Mnamo mwaka wa 2022, Misri ilianza kujenga kinu cha nyuklia cha El-Dabaa, kituo cha kwanza cha nyuklia nchini humo, ambacho kiko katika jimbo la Mediterania takriban kilomita 300 kaskazini magharibi mwa Cairo.

Mpango huo unatokana na makubaliano kati ya Misri na Russia. Takriban dola bilioni 25, sawa na asilimi 85 ya gharama ya ujenzi ukiwa ni mkopo uliotolewa na Russia kwa Misri kwa ajili ya ujenzi wa kinu hicho.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha