UNESCO yazindua mradi wa kusaidia elimu ya ufundi stadi inayohusiana na utamaduni nchini Tanzania

(CRI Online) Novemba 10, 2023

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) likishirikiana na shirika moja lisilo la kiserikali la Saudi Arabia, limezindua mradi nchini Tanzania unaolenga kusaidia elimu na mafunzo ya ufundi stadi yanayohusiana na utamaduni.

Mradi huo unalenga kuhimiza maendeleo ya kijamii kupitia mafunzo na elimu ya ufundi stadi na ajira zinazohusiana na utamaduni nchini Tanzania, taarifa ya UNESCO imesema huku ikiongeza kuwa mradi huo utakaotekelezwa kati ya mwaka 2023 na 2025, utahimiza maendeleo endelevu ya sekta ya utamaduni na ubunifu nchini Tanzania kupitia kuimarishwa kwa upatikanaji wa elimu na mafunzo yanayohusiana na utamaduni.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha