Rais Xi Jinping asisitiza kujenga China Nzuri na kukamilisha mfumo wa usimamizi wa nguvu asilia ya udhibiti wa vipengele vya kazi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 08, 2023

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumanne alipokuwa akiongoza mkutano wa tatu wa Kamati ya Taifa ya Maendeleo na Mageuzi ya Kina ya China ameagiza kufanyika juhudi za kuhimiza kwa pande zote ujenzi wa China Nzuri na kukamilisha mfumo wa usimamizi wa nguvu asilia ya udhibiti wa vipengele vya kazi (Natural Monopoly).

Mkutano huo umepitia na kupitisha miongozo kadhaa. Miongozo hiyo ni pamoja na kuhamasisha ujenzi wa China Nzuri katika mambo yote, kukamilisha mfumo wa bajeti ya uendeshaji wa mtaji wa kiserikai, kukamilisha mfumo wa usimamizi wa nguvu asilia ya udhibiti wa vipengele vya kazi (Natural Monopoly), kuimarisha usimamizi wa wataalamu wanaoshiriki katika kufanya maamuzi ya mambo ya kiumma, na kuimarisha usimamizi na udhibiti maalum wa mikoa wa mazingira ya kiikolojia.

Rais Xi, ambaye ni mkurugenzi wa kamati hiyo amesema kuwa kujenga China Nzuri ni kazi muhimu ya kujenga nchi ya kijamaa yenye maendeleo ya mambo ya kisasa katika sekta zote. Amehimiza juhudi za kimsingi kukamilisha lengo la kujenga China Nzuri ifikapo Mwaka 2035.

Rais Xi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), pia ametoa wito wa kuimarishwa kwa usimamizi juu ya wataalamu wanaoshiriki katika maamuzi ya mambo ya kiumma na kujenga mazingira ya kuvutia wataalamu wenye ujuzi, nguvu na kufuata maadili kushiriki katika kufanya maamuzi ya mambo ya kiumma, na kuwawezesha watoe mchango ipasavyo.

“Kwa mujibu wa mahitaji mapya ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ni muhimu kufanya juhudi zaidi za kushughulikia masuala ya kiikolojia na mazingira, kujenga ustaarabu wa ikolojia, na kutumia kikamilifu nafasi ya vinara na watu wa mifano,” kwa mujibu wa mkutano huo.

Mkutano huo umesisitiza juhudi za kuhimiza uwekezaji zaidi kutoka kwenye mtaji wa kiserikali katika viwanda na sekta muhimu ambazo zina nguvu ya ushawishi katika uhai wa uchumi wa nchi na usalama wa nchi, pamoja na sekta za huduma za kiumma, uwezo wa kukabiliana na dharura, na ustawi wa umma unaohusu maendeleo ya taifa na ustawi wa watu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha