Rais Xi Jinping asema ushirikiano wa miji dada ya China na Marekani una matunda makubwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 03, 2023

Beijing - Rais wa China Xi Jinping ametuma ujumbe kwa ajili ya Mkutano wa Tano wa Miji dada ya China na Marekani akisema ushirikiano wa karibu kati ya mikoa/majimbo dada na miji dada umekuwa na matunda katika miongo minne iliyopita.

Msingi wa uhusiano kati ya China na Marekani upo kwa watu na chanzo cha nguvu kinatokana na urafiki kati ya watu, Rais Xi amesema leo Ijumaa katika ujumbe wake kwenye mkutano huo unaofanyika Suzhou, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China.

Mikoa/majimbo dada na miji dada ni majukwaa muhimu ya kuimarisha urafiki na kufikia ushirikiano wa mafanikio, Rais Xi amesema, huku akibainisha kuwa jozi 284 za miji dada na majimbo/mikoa dada zimeundwa tangu jozi ya kwanza ilipoanzishwa Mwaka 1979.

“Mikoa/majimbo dada na miji dada imeshiriki katika ushirikiano wa karibu, wenye tija katika miongo minne iliyopita, na kuleta manufaa yanayoonekana kwa watu wa pande zote mbili” Rais Xi amesema.

Amesisitiza kuwa Mkutano wa Miji dada ya China na Marekani ni utaratibu muhimu wa mabadilishano kati ya miji na umekuwa na jukumu chanya katika kuhimiza maendeleo na ushirikiano kati ya miji dada.

Amewataka washiriki wa mkutano huo kuendelea kutumika mabadilishano kati ya miji kama daraja, ili kuwezesha mikoa/majimbo na miji kuchukua nafasi kubwa zaidi katika kuendeleza uhusiano kati ya pande mbili kuwa mzuri na thabiti, na kuboresha ustawi wa watu wa nchi hizo mbili.

Mkutano huo wenye kaulimbiu ya "Jenga Miji ya Kijani kwa ajili ya Watu," umeandaliwa kwa pamoja na Shirikisho la Watu wa China kwa Urafiki na Nchi za Ng’ambo na serikali ya Mkoa wa Jiangsu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha