

Lugha Nyingine
Rais Xi akutana na Gavana wa Jimbo la California, Marekani
Rais Xi Jinping wa China amekutana na Gavana wa Jimbo la California la Marekani, Gavin Newsom, katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing ambapo katika mazungumzo yao siku ya Jumatano Rais Xi amesema China na Marekani, zikiwa nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani, zinachangia zaidi ya theluthi moja ya uchumi wa dunia na karibu robo ya watu wote duniani, huku biashara kati ya nchi hizo mbili ikiwa ni takriban moja ya tano ya jumla ya uchumi wa dunia, hivyo kufanya maslahi ya pande zote mbili kufungamana kwa karibu.
Rais Xi amebainisha kuwa mafanikio ya uhusiano kati ya China na Marekani hayakuja kwa urahisi na yanapaswa kuthaminiwa zaidi. Sera ya China kuhusu Marekani ni thabiti, ambayo ni kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na kunufaishana, na kuongeza kuwa China itaendelea kufanya kazi katika mwelekeo huu ikitumai Marekani itashirikiana na China katika mwelekeo huo huo.
Naye Gavana Newsom amesema, katika miongo michache iliyopita, China imepata mafanikio makubwa katika maendeleo, hasa katika nyanja ya nishati mpya. Amesisitiza kuwa hakuna uhusiano mwingine wa nchi mbili ambao ni muhimu zaidi kuliko huu kati ya Marekani na China, na uhusiano huu ni muhimu kwa mustakabali wa Marekani na unahusu ustawi wa watu wake.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma