

Lugha Nyingine
Rais wa China ajibu barua ya Mwenyekiti wa Mfuko wa urithi wa anga kati ya Marekani na China na askari wastaafu wa Flying Tigers
Rais Xi Jinping wa China amejibu barua ya Mwenyekiti wa Mfuko wa Urithi wa Anga kati ya Marekani na China Jeffrey Greene na askari wastaafu wa Flying Tigers, Harry Moyer na Mel McMullen.
Katika barua hiyo, Rais Xi amesema, alitiwa moyo na shauku kubwa kuona mfuko huo na askari wastaafu wa Flying Tigers wanawezesha Wachina na Wamarekani wengi kujua kuhusu simulizi za Flying Tigers kwa muda mrefu, na kwa kuhamasishwa na juhudi hizi vijana na watoto wengi nchini Marekani wamejiunga kwenye “Shule ya urafiki ya Flying Tigers” na “Programu ya Viongozi Vjana”.
Huku akibainisha kuwa "katika kukuza uhusiano kati ya China na Marekani, matumaini yapo kwa watu, msingi upo miongoni mwa watu, na mustakabali uko kwa vijana," Rais Xi amesema maendeleo tulivu ya uhusiano kati ya China na Marekani kwenye zama mpya yanahitaji juhudi na kuungwa mkono na kizazi kipya cha Flying Tigers.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma