Rais Xi Jinping atoa wito wa utayari imara wa kupigana vita kwa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 11, 2023

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu alipokagua Jeshi la Kundi la 78, Septemba 8, 2023. (Xinhua/Li Gang)

HARBIN - Rais wa China Xi Jinping ametoa wito wa kuimarishwa kwa kila idara utayari wa vikosi vya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) kupigana na kushinda vita wakati wa ukaguzi wa Jeshi la Kundi la 78 lenye makao yake makuu kaskazini mashariki mwa China siku ya Ijumaa.

Rais Xi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amekutana na wajumbe wa jeshi la kundi hilo na kupiga picha nao. Amelipongeza jeshi na polisi wabeba silaha kwa ushiriki wao wa haraka na shupavu katika kazi ya kutoa msaada wakati mafuriko yalipokumba mikoa ya kaskazini na kaskazini mashariki mwa China.

Rais Xi ametaka kufanyika juhudi za kuboresha kiwango cha utayari wa kupigana vita na kushinda, kuimarisha mafunzo ya masomo muhimu na magumu, na kujenga uwezo mpya wa kivita.

Amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ujenzi wa chama, kudumisha kiwango cha juu cha uadilifu na mshikamano wa jeshi, na kuhakikisha kiwango cha juu cha utulivu na usalama wa jeshi.

Zhang Youxia na maofisa wengine waandamizi wa kijeshi walikuwepo wakati wa ukaguzi huo. 

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akikutana na wajumbe wa Jeshi la Kundi la 78, alipokagua Jeshi la Kundi la 78, Septemba 8, 2023. (Xinhua/Li Gang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha