Namibia yazindua mradi wa majaribio wa baiskeli ili kuanzisha usafiri wenye gharama nafuu na matumizi mazuri ya nishati

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 01, 2023

Mtu huyu akipiga picha pamoja na baiskeli inayotumia nishati ya umeme mjini Windhoek, Namibia, Agosti 31, 2023. (Picha na Musa C Kaseke/Xinhua)

Mtu huyu akipiga picha pamoja na baiskeli inayotumia nishati ya umeme mjini Windhoek, Namibia, Agosti 31, 2023. (Picha na Musa C Kaseke/Xinhua)

WINDHOEK - Namibia siku ya Alhamisi imezindua mradi wa majaribio wa baiskeli unaolenga kuanzisha suluhu za usafiri wa bei nafuu na matumizi mazuri ya nishati kupitia matumizi ya baiskeli zinazotumia nishati ya umeme.

Mradi wa majaribio wa EBikes4Windhoek, ambao ni mpango wa mji mkuu wa nchi hiyo, Windhoek, umewekwa ili kuhimiza machaguo ya usafiri endelevu na kuimarisha upatikanaji na mwonekano wa baiskeli mjini.

Mradi huo wa majaribio utahusisha ushiriki wa wanafunzi 18 kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Namibia na wanafunzi 18 kutoka Chuo Kikuu cha Namibia, ambao walichaguliwa kupitia mchakato mkali wa maombi.

Wanafunzi hawa watashiriki kikamilifu katika mradi huo kwa muda wa miezi mitatu na kuendelea kumiliki baiskeli zinazotumia nishati ya umeme katika kipindi hiki na timu ya mradi itatathmini ufanisi wa kuendesha baiskeli katika usafiri wa kila siku, kutathmini hatua za usalama, na kulinganisha gharama za usafiri kwa wanafunzi wanaoshiriki.

Ikiwa mradi huo wa majaribio utafanikiwa, mamlaka husika za manispaa zitachunguza uwezekano wa kupanua matumizi ya baiskeli kwa watu wengi zaidi.

Magari yanayotumia nishati mbadala na njia nyingine za usafiri za kutumia nishati ya umeme "zina uwezekano wa kuchagiza mustakabali wa usafiri nchini Namibia -- kuchukua nafasi ya magari ya zamani yanayotumia mafuta ya kawaida," Meya wa Windhoek Joseph Uapingene amesema kwenye hafla ya uzinduzi.

Baiskeli hizo zinazotumia umeme (E-Bike) zina vifaa vya betri na injini ili kutoa usaidizi wa ziada kwa waendeshaji, na kuzifanya ziwe bora kwa kupita ardhi ya milima ya Windhoek, kutafika umbali mrefu au kukabiliana na hali ya hewa ya joto, ambavyo vyote ni vya kawaida katika eneo hilo.

Kwa sasa, kuna machaguo machache kwa usafiri wa umma, na kaya za kipato cha chini huko Windhoek hutenga hadi robo ya mapato yao kwa ajili ya gharama za usafiri, kwa mujibu wa serikali ya manispaa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha