

Lugha Nyingine
Tamasha la Kwanza la Teknolojia za Akili Bandia lafanyika Beijing
BEIJING- Jumatatu wiki hii Tamasha la Kwanza la Teknolojia za Akili Bandia (AI) limefanyika kwenye Jengo la Vyombo vipya vya Habari la Kampuni ya Gazeti la People's Daily, mjini Beijing, China.
Wanafunzi wa Chuo cha Opera ya Kijadi cha China wakishirikiana na msanii wa kidijitali Mu Lan kutumbuiza "New Dingjun Mountain" Agosti 28, 2023, mjini Beijing, China. (Picha na Huangfu Wanli)
Kupitia vipindi mbalimbali vya kisanii vilivyojaa teknolojia mpya na teknolojia za akili bandia, tamasha hilo limeonyesha matokeo ya hali ya juu na uwezo katika sekta ya teknolojia za akili bandia (AI).
Vipindi vyote katika tamasha hilo vimebuniwa na kuandaliwa kwa AI, na sehemu nyingine kama vile mialiko, tiketi za kuingia, na mabango yalikamilishwa kwa ushirikiano wa kompyuta na binadamu, ikionyesha muunganisho mzuri kati ya teknolojia na watu.
Kwenye tamasha hilo, picha ya kidijitali ya programu ya kutafuta video mtandaoni "Baize" ilionyeshwa kwa mara ya kwanza. Hii ni programu ya kutafuta video mtandaoni zenye miundo mbalimbali iliyotolewa kwa pamoja na Maabara ya Kitaifa ya Utambuzi wa Maudhui ya Mawasiliano na Sayansi na kampuni ya Renminzhongke, na hufanya mazungumzo yanayovuka muda na nafasi kwa kutumia taswira ya kijana.
Picha ya kidijitali ya "Bai Ze" ikionekana kwa mara ya kwanza kwenye tamasha hilo. (Picha na Li Danyang)
Teknolojia ya kidijitali hutumia kwa kuvuka muda na nafasi, ikionyesha mambo hayajatokea na yaliyopita. "Mandhari ya Majira Manne katika Kasri la Kale la Majira ya Joto" (Summer Palace) lililoko Mji wa Beijing yanaonyesha tena hazina ya kihistoria ya "Kasri la Kale la Majira ya Joto" kwa kutumia teknolojia ya dijitali ya 720° VR 8K, iliyowezeshwa na kionyeshi chembamba na chepesi cha kichwa cha VR na kifaa cha kunasa sauti cha kuvaa shingoni cha kidijitali, na kuleta uzoefu wa aina yake kwa watazamaji.
Timu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kaskazini-Mashariki cha China ikiwasilisha "Mashindano ya Mashine ya Super Confrontation ". (Picha na Sun Haifeng)
Katika "Mashindano ya Mashine ya Super Confrontation ", "Timu ya Ubunifu wa Roboti ya T-DT" ya Chuo Kikuu cha Kaskazini-Mashariki iliunganisha kikamilifu maono ya kimashine, ubunifu wa mfumo uliopachikwa, udhibiti wa mitambo, urambazaji usio na nguvu, mwingiliano wa kompyuta na binadamu na teknolojia zingine, na kuonyesha uwezo wa uchunguzi na busara wa vijana katika sayansi na teknolojia.
Watu wakiwa kwenye picha moja iliyopigwa katika maeneo mbalimbali. (Picha na Weng Qiyu)
Aidha, tamasha hilo pia limehusisha maonyesho ya roboti ya panda, mwongozo wa "binadamu wa kidijitali", maonyesho ya drone wakati wa usiku, nk, hali ambayo imeonyesha kikamilifu uzuri wa binadamu na teknolojia, na pia imeonyesha uwezekano usio na kikomo wa teknolojia ya akili ya bandia katika siku za baadaye.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma