Rais Xi Jinping ahimiza kuchukuliwa hatua ili kuifanya jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja kuwa uhalisia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 23, 2023

Mtu akipiga picha kwenye kituo cha vyombo vya habari cha Mkutano wa 15 wa viongozi wakuu wa  nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 21, 2023. (Xinhua/Li Yahui)

Mtu akipiga picha kwenye kituo cha vyombo vya habari cha Mkutano wa 15 wa viongozi wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 21, 2023. (Xinhua/Li Yahui)

JOHANNESBURG - Rais wa China Xi Jinping ametoa wito wa kuchukuliwa hatua ili kutafsiri maono ya jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja kuwa uhalisia.

Wito huo wa Rais Xi umetolewa siku ya Jumanne katika hotuba ya maandishi iliyosomwa na Waziri wa Biashara wa China Wang Wentao kwenye Baraza la Viwanda na Biashara la BRICS 2023.

"Hivi sasa, mabadiliko duniani, katika zama tulizonazo na katika historia yanajitokeza kwa namna ambayo haijawahi kutokea hapo awali, na kuleta jamii ya binadamu katika wakati muhimu," Rais Xi ameonya katika hotuba iliyopewa jina la Kuimarisha Mshikamano na Ushirikiano ili Kushinda Hatari na Changamoto na Kujenga kwa Pamoja Dunia nzuri zaidi.

"Je, tufuate ushirikiano na muunganisho, au tujisalimishe tu katika migawanyiko na mapambano? Je, tunapaswa kufanya kazi pamoja ili kudumisha amani na utulivu, au tulale na kutembea kwenye shimo la Vita Baridi? Je, tunapaswa kukumbatia ustawi, uwazi na ujumuishaji, au kuruhusu umwamba na vitendo vya ukandamizaji ili kutuweka katika mfadhaiko? Je, tuzidishe kuaminiana kupitia mawasiliano na kufunzana, au turuhusu kiburi na upendeleo vifumbe dhamiri?" Rais Xi ameuliza. "Lengo la historia litafikiwa kwa machaguo tunayofanya."

Dunia yetu ya leo imekuwa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ambapo sote tuna mchango mkubwa wa kuendelea kuishi, Rais Xi amesema, huku akieleza kwamba kile ambacho watu katika nchi mbalimbali wanatamani “kwa hakika si Vita Baridi vipya au kambi ndogo maalum; wanachokitaka ni Dunia iliyo wazi, jumuishi, safi na mzuri ambayo inafurahia amani ya kudumu, usalama wa wote na ustawi wa pamoja."

"Kila nchi ina haki ya kupata maendeleo, na watu katika kila nchi wana uhuru wa kutafuta maisha ya furaha," Rais Xi amesema, huku akisisitiza kuwa China itashirikiana na nchi nyingine zote katika kuharakisha ushirikiano chini ya Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, kukabiliana na changamoto za pamoja na kufanya maisha kuwa bora kwa watu kote duniani.

Huku akitoa wito wa uhakikisho wa usalama kwa wote na kutoa mwaliko kwa nchi zote kuunga mkono na kufuata Pendekezo la Usalama wa Dunia la China, Rais Xi pia amesisitiza haja ya kujitolea katika mawasiliano na kufundishana kati ya ustaarabu mbalimbnali, na pia amekaribisha nchi nyingine zote kushiriki katika ushirikiano chini ya Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia.

Rais Xi pia amezungumza kuhusu kuunda ushirikiano wa kimkakati wenye nguvu zaidi wa nchi za BRICS, kupanua muundo wa 'BRICS Plus', kuendelea kuhimiza upanuzi wa wanachama, kuimarisha mshikamano na ushirikiano na nchi nyingine zenye masoko yanayoibukia na zile zinazoendelea, kuhimiza uwepo wa ncha nyingi duniani na demokrasia zaidi katika uhusiano wa kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha