Mradi wa China wa kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo nchini Afrika Kusini wanufaisha maeneo ya makazi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 22, 2023

Chanzo: Xinhua

Jenereta iliyotolewa na Kampuni ya Longyuan SA ikionekana katika ua kwenye makazi ya wazee huko De Aar, Afrika Kusini, Agosti 10, 2023. (Xinhua/Dong Jianghui)

Jenereta iliyotolewa na Kampuni ya Longyuan SA ikionekana katika ua kwenye makazi ya wazee huko De Aar, Afrika Kusini, Agosti 10, 2023. (Xinhua/Dong Jianghui)

CAPE TOWN – Kila asubuhi ya Saa 12:30 huko De Aar, mji mdogo ulioko umbali wa zaidi ya kilomita 750 Kaskazini-Mashariki mwa Cape Town, mji mkuu wa bunge wa Afrika Kusini, Deswin Basson husimama kwenye mlango wa nyumba yake kwenye upepo wenye baridi, akingojea wenzake kumchukua na kumpeleka kazini kwenye kituo cha kupozea umeme kilicho umbali wa zaidi ya kilomita 20.

Ingawa kuamka mapema siyo jambo la kufurahisha kila wakati, mwenyeji huyo wa mji huo mwenye umri wa miaka 27 amejaa shauku kila siku. Deswin anafanya kazi kwenye kituo cha transfoma cha Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Upepo wa De Aar wa Kampuni ya Nishati Mbadala ya Longyuan, Tawi la Afrika Kusini (Longyuan SA).

Ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kuwa mradi huo ndiyo uliobadilisha maisha yake. "Kwa kweli ninaamini kwamba, bila wao, nisingekuwa nilivyo leo," amesema.

Mradi huo unapatikana karibu na De Aar katika Jimbo la Kaskazini la Cape la Afrika Kusini, ambalo lina chanzo kikubwa cha upepo. Mradi huu ulikamilishwa na kuanza kutumika Mwaka 2017 na Kampuni ya Longyuan SA, kampuni tanzu inayomilikiwa kikamilifu na kampuni tanzu ya Kundi la Kampuni za Uwekezaji wa Nishati la China (CHN Energy) Kundi la Kampuni za Nishati za Longyuan la China (Longyuan Power), kwa uwekezaji wenye thamani ya takriban jumla ya Yuan bilioni 2.5 (sawa na Dola za Kimarekani milioni 343) na jumla ya uwezo uliowekwa wa MW 244.5.

Pamoja na kuendelea kuipatia maeneo ya makazi umeme tulivu na safi wenye nguvu ya takriban KWH milioni 760 kila mwaka, kampuni hiyo ikiwa kampuni ya China ya ng’ambo haijaacha jitihada yoyote katika kutimiza wajibu wake wa kijamii, na imetoa msaada kwa wenyeji wa huko.

Kwa mfano, inatoa zaidi ya randi milioni 4.5 kila mwaka (kama dola 236,100) kwa mpango wa ufadhili wa masomo, ambao hadi sasa umefadhili wanafunzi 112 wa vyuo vikuu nchini Afrika Kusini kumaliza masomo yao.

Deswin ni mmoja wao. "Kwa muda mrefu kama naweza kukumbuka, nilitaka kuwa mhandisi," ameliambia Xinhua. Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, Deswin alijiunga rasmi na Kampuni ya Longyuan SA Mwezi Aprili mwaka jana, na kuwa sehemu ya timu yake ya uendeshaji na ukarabati.

Hadi kufikia sasa, mradi huo wa umeme umetoa nafasi za kazi zaidi ya 700 kwa wenyeji wa huko na kusaidia kuboresha hali ya maisha ya watu wa eneo hilo.

Picha hii iliyopigwa Agosti 10, 2023 ikionyesha mashine za kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo na njia za kusambaza umeme za Mradi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo wa De Aar wa Kampuni ya Longyuan SA huko De Aar, Afrika Kusini. (Xinhua/Dong Jianghui)

Picha hii iliyopigwa Agosti 11, 2023 ikionyesha mradi wa maji chini ya ardhi ni uliojengwa na Kampuni ya Longyuan SA huko De Aar, Afrika Kusini. (Xinhua/Dong Jianghui)

Picha hii iliyopigwa Agosti 11, 2023 ikionyesha mradi wa maji chini ya ardhi ni uliojengwa na Kampuni ya Longyuan SA huko De Aar, Afrika Kusini. (Xinhua/Dong Jianghui)

Wanafunzi wakicheza mpira wa miguu kwenye uwanja uliokarabatiwa na Longyuan SA mjini De Aar, Afrika Kusini, Agosti 10, 2023. (Xinhua/Dong Jianghui)

Wanafunzi wakicheza mpira wa miguu kwenye uwanja uliokarabatiwa na Longyuan SA mjini De Aar, Afrika Kusini, Agosti 10, 2023. (Xinhua/Dong Jianghui)

Daktari wa meno Teboho Mpotle akifanya kazi kwenye basi la matibabu lililonunuliwa na Kampuni ya Longyuan SA huko De Aar, Afrika Kusini, Agosti 10, 2023. (Xinhua/Dong Jianghui)

Daktari wa meno Teboho Mpotle akifanya kazi kwenye basi la matibabu lililonunuliwa na Kampuni ya Longyuan SA huko De Aar, Afrika Kusini, Agosti 10, 2023. (Xinhua/Dong Jianghui)

Daswin Basson (kushoto) na Regardt van Tonder, Naibu Meneja wa Kituo cha transfoma cha Mradi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo wa De Aar wa Kampuni ya Longyuan SA wakifanya kazi kwenye kituo hicho huko De Aar, Afrika Kusini, Agosti 10, 2023. (Xinhua/Dong Jianghui)

Picha hii iliyopigwa Agosti 10, 2023 ikionyesha Kituo cha Kupozea Umeme cha Mradi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo wa De Aar wa Kampuni ya Longyuan SA huko De Aar, Afrika Kusini. (Xinhua/Dong Jianghui)

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha