

Lugha Nyingine
Wanasayansi wa China wafanikiwa kupata sukari ya hexose kwa hewa ya kaboni
Picha hii iliyopigwa tarehe 13, Agosti, 2023 ikionesha sampuli ya sukari ya Hexose ya majimaji kwenye Idara ya Utafiti wa Teknolojia ya Biolojia ya Kiviwanda ya Tianjin chini ya Taasisi kuu ya Sayansi ya China (CAS) huko Tianjin, Kaskazini mwa China (Xinhua/Sun Fanyue)
Wanasayansi wa China wamevumbua njia ya kutumia hewa ya kaboni (CO2) katika mazingira ya maabara kutengeneza sukari ya hexose, ambayo ni aina ya sukari inayohusiana moja kwa moja na kimetaboliki ya lishe ya mwili. Mafanikio hayo ni hatua muhimu katika maendeleo ya dunia ya kutengeneza sukari kwa njia ya kibinadamu.
Utafiti ulioleta njia hiyo mpya ulifanywa na Idara ya utafiti wa Tekonolojia ya Biolojia ya Kiviwanda ya Tianjin pamoja na Idara ya utafiti wa Kemikali-Fizikia ya Dalian, ambazo zote ni chini ya Taasisi kuu ya Sayansi ya China (CAS). Matokeo hayo ya utafiti yalichapishwa Jumatano kwenye tovuti ya jarida la “Science Bulletin”.
Timu hiyo ya utafiti ilisema kuwa, kuhuisha jukwaa la “CO2-Sukari” kwa njia ya kibinadamu kuna umuhimu mkubwa kwa kutatua changamoto ya utoaji wa sukari kwa chakula kutokana na upungufu wa ardhi na mabadiliko ya tabianchi.
Timu hiyo imesema, Jukwaa hilo la kemikali -biolojia limethibitishwa kuwa na ufanisi mkubwa zaidi kuliko njia ya jadi ya ubadilishaji wa hewa ya kaboni.
Wanasayansi wakifanya majaribio kwenye maabara ya Idara ya utafiti wa Teknolojia ya Biolojia ya ya Kiviwanda ya Tianjin chini ya CAS huko Tianjin, China, tarehe 13, Agosti, 2023. (Xinhua/Sun Fanyue)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma