China yaongeza matumizi ya kina wa TEHAMA katika sekta ya usafirishaji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 14, 2023

China inafanya juhudi kubwa kukuza ujumuishaji wa kina wa TEHAMA (IT) kwenye sekta ya usafirishaji. Huku bidhaa mpya na aina mpya za biashara zikiendelea kujitokeza, watu nchini China wananufaika kutokana na kuboreshwa kwa huduma za usafiri katika pande mbalimbali, kutoka barabara za mijini hadi barabara kuu kati ya miji.

Kwenye majira ya joto ya mwaka huu, watu wengi nchini China wamegundua kuwa programu za kwenye simu zenye ramani zinaweza kuonyesha njia zenye vivuli vya "kukinga dhidi ya jua" kwa watembea kwa miguu katika muda halisi, na kupendekeza njia yenye kivuli kulingana na mahali anakokwenda mtumiaji.

Abiria wakishuka kwenye basi linalojiendesha katika wilaya ya Deqing, mjini Huzhou, Zhejiang mashariki mwa China. (People's Daily Online / Xie Shangguo)

Abiria wakishuka kwenye basi linalojiendesha katika wilaya ya Deqing, mjini Huzhou, Zhejiang mashariki mwa China. (People's Daily Online / Xie Shangguo)

Ofisa mkuu mtendaji wa kampuni ya ramani ya Amap ya China, Bw. Li amesema kwa kutumia teknolojia ya kutambua kwa mbali, programu yao inaweza kutambua uwepo wa miti karibu na barabara, na kutambua uwepo wa mwanga na hali ya kivuli ya sehemu za barabara katika maeneo mbalimbali.

Kutokana na matumizi ya teknolojia za kisasa za simu za mkononi, huduma za usafirishaji mijini nchini China zimeboreshwa sana na kuwa na ufanisi mkubwa.

Bwana Li amesema kuna wakati ni vigumu kupata teksi na wakati mwingine si vigumu, lakini muda wa kusubiri teksi huongezeka wakati wa msongamano.

Bwana Li pia amesema katika juhudi za kuboresha ufanisi kulingana na mahitaji, kampuni ya Amap imeongeza data kubwa ili kutabiri msongamano na kurekebisha bei kwa wakati halisi.

Magari ya kusafisha barabarani yanayojiendesha yakiwa kazini katika mtaa wa mji wa Ordos, mkoa wa Mongolia ya Ndani, China. (People's Daily Online/Wang Zheng)

Magari ya kusafisha barabarani yanayojiendesha yakiwa kazini katika mtaa wa mji wa Ordos, mkoa wa Mongolia ya Ndani, China. (People's Daily Online/Wang Zheng)

Takwimu zilizotolewa na wizara ya Uchukuzi ya China (MOT) zinaonyesha kuwa zaidi ya miji 300 ina huduma za kuita taxi kwa njia ya simu, na oda zaidi ya milioni 25 kila siku, na jumla ya baiskeli za kuchangia milioni 15 zimesambazwa kote nchini, zikiwa na watumiaji zaidi ya milioni 28 kila siku.

Ofisa wa idara ya sayansi na teknolojia ya wizara hiyo amesema maendeleo ya kasi ya kiuchumi yamechochea mahitaji zaidi ya usafiri, lakini wakati huo huo yameleta changamoto kama vile msongamano, ajali na uchafuzi wa mazingira. Amesema TEHAMA ikiwakilishwa na akili ya bandia (AI), inaweza kutoa mbinu mpya za kuimarisha uwezo wa huduma wa miundombinu ya usafiri.

Kwa kujenga na kuvifanyia mabadiliko vifaa vinavyotumia teknolojia ya akili bandia, vinavyowezesha kuendana na mabadiliko mtiririko wa usafiri wa magari yanayotokea kwa wakati halisi kwenye makutano ya 332, ya Eneo la maendeleo ya Kiuchumi na Kiteknolojia la Beijing, ambalo pia linajulikana kama mji wa kieletetroniki, eneo hilo limekuwa na matokeo ya kushangaza katika kukabiliana na msongamano wa magari.

Vifaa vya teknolojia ya akili bandia vimepunguza urefu wa foleni kwa asilimia 30.3 na muda usio wa lazima wa taa za kijani kwa asilimia 18.33 katika baadhi ya maeneo.

Picha inaonyesha kituo cha usimamizi cha eneo jipya la Rongjiang katika mji wa Ganzhou, mkoani Jiangxi, Mashariki mwa China. (People's Daily Online/Zhong Wanshan)

Picha inaonyesha kituo cha usimamizi cha eneo jipya la Rongjiang katika mji wa Ganzhou, mkoani Jiangxi, Mashariki mwa China. (People's Daily Online/Zhong Wanshan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha